ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 15, 2013

Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA, Soweto, Arusha

Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali ya Seliani na Mount Meru.

Bomu hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.

Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.

Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA.

ILANI: Baadhi ya picha zilizopachikwa hapo huenda zikagusa hisia ya mtizamaji, tafadhali ikiwa huwezi kuvumilia kuona damu usibofye tarakimu zilizopo hapo chini kufungua picha zinazofuatia.
kwa picha zaidi bofya read more








2 comments:

Anonymous said...

Tanzania sasa imegeuka Rwanda??!! lakini ili haki ipatikane lazima damu imwagike. Poleni sana.

Anonymous said...

Si maji ni DAMU ya watanzania wazalendo na wananchi wenye nchi ya AMANI na wanaomcha MUNGU!Mungu ni wewe ulituumba na ni wewe tu unaejua thamani ya mwanadamu wala si mwanadamu mwenzie,hivyo tunakuomba upigane vita hivi wewe mwenyewe kwani unaona jinsi wengine walivyokuwa simba wala watu bila chembe ya huruma!Laukana Baba wa taifa angefufuka aone hayaa!!!!!!!!!!