ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 21, 2013

KAJALA NA WEMA KIMENUKA HAPAPIKIKI WALA HAPALIKI PITIA HII HABARI

Wema katika pozi na Kajala.
Na Musa Mateja
KIMENUKA! Utabiri wa wengi kuwa ushosti wa waigizaji masistaduu wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja kutumbukia nyongo unadaiwa kutimia na sasa wametibuana, Ijumaa limenyetishiwa.

Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu (jina linahifadhiwa), mwanzoni baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya Sh. milioni 13 na kumnusuru kutokwenda Segerea a.k.a Segedansi, wawili hao walikuwa marafiki kama pete na kidole.

SIKU KAMA HIZI
“Walishinda wote, walilala wote, walikwenda klabu wote yaani Kajala alikuwa anamnyenyekea ‘madam’ Wema kwa kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Kuna wakati hapa katikati Kajala alikuwa kama katibu muhtasi wa madam, si unajua lazima atumikie fedha za watu?
“Kabla hajaenda Mwanza kwa ajili ya mapumziko kwa bibi zake, nilimsikia Kajala akilalama kuwa madam aliamka siku moja akawa amemchunia, unaambiwa hata salamu ikawa hakuna.

Wema akimlisha keki Kajala wakati wa sherehe ya kumkaribisha uraiani.

TATIZO NI WAPAMBE
“Hapo ndiyo maneno ya pembeni yakaanza kwa sababu mbali na Kajala, Wema pia ana wapambe wengine na mbali na Wema, Kajala naye ana kampani. Kwa hiyo sosi ya manenomaneno ni hizo kampani zao.
“Ipo siku kabisa Wema alimlalamikia Kajala hadharani kuwa amekuwa akimsema vibaya kwa watu.
“Yale maneno yalimuuma sana Kajala, ikabidi arudi nyumbani kwao lakini akawa anaogopa kumwambia mama yake kuwa ametibuana na Wema hadi alipotimkia Mwanza.

KUMBE ALIMKOSESHA DILI?
“Lakini kabla ya hii ishu ya kulaumiana, kipindi cha nyuma kidogo Kajala alipata dili la kwenda kurekodi filamu nchini China na mastaa wengine lakini ikadaiwa kuwa Wema alichomoa hivyo mwigizaji huyo hakwenda pamoja na kwamba alishapewa baraka zote na baba yake.
“Unaambiwa alikuwa amekamilisha taratibu zote za kwenda China, hadi tiketi alikuwa ameshakata lakini suala hilo lilipotua kwa Wema, ilidaiwa kuwa alikataa kumruhusu.

TATIZO MILIONI 13?
“Mimi nakwambia zile milioni 13 zinamkosesha raha Kajala hadi unamuona kabisa kwamba ana stress (msongo wa mawazo). 
“Wewe fikiria, kazi inayomwingizia mkwanja ni filamu, sasa unaambiwa inadaiwa kuwa madam hataki acheze filamu za watu wengine, sasa ataishije jamani?

SASA NI KUNUNIANA KWA KWENDA MBELE
“Mimi nakwambia ndiyo maana ameamua kwenda kupumzika Mwanza baada ya kuwa wananuniana kwa kwenda mbele.”
Baada ya kupata habari hizo, Ijumaa lilimtafuta Wema kwa njia ya kilongalonga chake cha kiganjani ili kupata undani wa sakata hilo lakini hakupatikana hewani.

NYUMBANI KWA WEMA
Baadaye mwanahabari wetu alisaga lami hadi kwa staa huyo Kijitonyama, Dar, alipogonga geti alitoka mlinzi aliyedai kuwa ‘malkia’ alikuwa ndani amelala na hakuhitaji usumbufu pamoja na kwamba ilikuwa saa 6:30 mchana.

MENEJA WAKE ANASEMAJE?
Hata hivyo, Ijumaa lilibisha hodi ofisini kwa Wema, Mwananyamala-Komakoma ili kuzungumza na meneja wake, Martin Kadinda ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli Kajala yupo Mwanza, aliomba ruhusa ya kwenda kupumzika tukampa. Hayo mengine ya kutibuana na madam siwezi kuyasemea kwa sababu yapo nje ya uwezo wangu.
“Lingekuwa ni suala la kazi hapo sawa lakini ni vizuri ukazungumza na mkurugenzi mwenyewe (Wema) lakini sidhani kama ataweza kuzungumza kwa sababu alikuwa anaumwa, amezidiwa na kupelekwa hospitali.”

WEMA ANAUMWA NINI?
Alipoulizwa Wema anaumwa nini, Kadinda alifunguka: “Sijajua lakini ugonjwa ni siri kati ya mhusika na daktari, cha msingi wewe ujue tu anaumwa.”

HUYU HAPA KAJALA
Baada ya kupita kote huko kusaka undani wa sakata hilo, Ijumaa lilimgeukia Kajala kwa njia ya simu ya mkononi akiwa jijini Mwanza na kumuuliza kulikoni kutibuana na Wema.
Huku sauti ikiwa chini, Kajala alisema: “Ni kweli kuna hali ambayo hata mimi mwenyewe nashindwa kuelewa lakini siwezi kuzungumzia kwa leo nikiamini yatapita.”

3 comments:

Anonymous said...

Kajala mdogo wangu nisikilize ninachokuambia, mie sikufahamu wala simfahamu Wema woote na wasoma tu kwenye magazeti. Nenda tafuta kazi hata kama ni ya bei ya chini au hata kama utafanya kazi mbili au tatu, mlipa hiyo hela kabisaa, Msaada wake usiwe chambo cha kukutesa na kukunyanyasa hata kidogo na wala usimnyenyekee. Wema anaonekana hawezi kuwa na rafiki maana ana penda kunyenyekewa masaa yoote. Hakika kukutoa jela ilikuwa jambo zuri sana na nchi nzimaa ikamwombea heri, sasa tena anakunyanyasa hiyo si haki wala ubinadamu hata kidogo. Kama unamsaidia mtu kwa moyo mmoja baasi unamsaidia unamwacha aendeleee na mambo yake sio kumyima raha na kumfanya mtumwa wako. Haijalishi umeongea kitu gani cha kumuuzi wala umefanya nini woote tu binadamu na mnaweza kaa mkayaongea sio anakurusha kama mpira kwa kuwa amekutoa jela. that is so not right. Poor Kajala, Mtumaini Mungu wako tu maana kwa Mungu yooote ya wezekana. Good luck..

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe mdau. Huo ndio ukweli. Kumsaidia mtu haimaanishi ndio awe mtumwa wako hata Mungu hapendi.

Anonymous said...

wema she is a spoil brats ndo maana kila leo anapata wanaume wa kumchezea chezea tu hapati wa kumuowa anadhani utoto wake udamumu mpaka kufa ndo maana kwa ajili ya kuwa spoil brats anaona anahaki ya kufanyia kila mtu mambo ya kijinga jinga na kitoto toto, nadhani anamatazizo ya akili achekiwe jamani na nahisi amekwenda kutoa mimba muhusika hataki mimba hiyo au

labda yeye mwenyewe si kicheche so unadhani maradhi gani au labda kapata duduz sikuobei mummy lakin punguza mikogo ya kijinga jinga unatakiwa ukuwe si mdogo tena wewe japo kwa mama ni mdogo

pole sana kajala natumai umejifunza na unajua wema vizuri hivi sasa achana naye anataka awe anaabudiwa kila siku kama mungu ndo maana diamond kaingia mitini