ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 2, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA JOPO LA WATAFITI WA MASUALA YA UCHUMI AFRIKA, JIJINI ARUSHA LEO

 Juu na chini ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa Jopo la Watafiti wa Masuala ya Uchumi Afrika (AERC) kujadili athari za Mazingira kwa Maendeleo ya Bara la Afrika, uliofanyika Jijini Arusha leo Juni 02, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mtafiti wa Kisayansi Kutoka Mpango wa Pamoja unaohusu Sera za Kisayansi na Mabadiliko ya Tabianchi, Keneth Strzepek (kulia) na Mtafiti Mwandamizi wa Kisayansi,Adam Schlosser (katikati) baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Jopo la Watafiti wa Masuala ya Uchumi Afrika (AERC) kujadili athari za Mazingira kwa Maendeleo ya Bara la Afrika, uliofanyika Jijini Arusha leo Juni 02, 2013.
 Profesa, Lemma Senbet, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) Terezya Huvisa, kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) Terezya Huvisa, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
 Juu na chini ni Baadhi ya washiriki wa mkutano huo waliohudhuria wakimsikiliza Makamu wa Rais
Picha na OMR

No comments: