Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Wizara ya Fedha kutoka
kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Christine Ngonyani akiwa na watumishi wa
wizara ya fedha akifafanua kuhusu mikopo inayotolewa na wizara ya fedha.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Bw. William Ghump
akifafanua jambo kuhusu Mkakati wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya
Fedha.
- Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Wizara ya Fedha kutoka kwa Mhasibu Ghana.Mkuu wa Serikali Bi. Christine Ngonyani akifafanua jambo kwa wananchi wa Ghana
Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma akijibu
swali kutoka kwa Mwanajeshi wa Ghana aliyekuwa anataka
kujua ni jinsi gani Wizara ya fedha inawasaidia wanajeshi ambao wanataka
kujikwamua kiuchumi.Wakushoto kwake ni Bw. Midladjy Maez(Mkatamiti) ambaye ni
Maneja wa Mahusiano TRL akisikiliza kwa makini maelezo hayo.
- Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Bi Christine Ngonyani akiwa na Miriam Mnzava kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Ingiahedi Mduma wakiwapatia huduma wakuu wa jeshi la Magereza la nchini Ghana.
Mkuu wa Kitengo
cha Mikopo Wizara ya Fedha kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Christine
Ngonyani akimpatia vipeperushi Bw. S.M Gyepi- Garbrah Mkuu wa Kitengo cha
Ukaguzi wa Ndani Ofisi ya Rais wa Ghana wakati wa Maadhimisho ya maonesho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma Nchini Ghana.
- Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Wizara ya Fedha kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Christine Ngonyani akiwa na watumishi wa wizara ya fedha walipotembelewa na Bw. Pascal Mugabe ambaye ni Afisa Tawala Rasilimali Watu wa Idara ya Utawala, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye yupo Nchini Ghana kwa masomo ya elimu ya juu(Phd) .
- Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani alipotembelea banda la Wizara ya fedha na kuelezea jinsi alivyofurahishwa na ushiriki wa Wizara ya fedha katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Mhe. Celina O. Kombani akisani kitabu cha wageni. Picha zote na Scola
Malinga – Hazina- Tanzania
No comments:
Post a Comment