ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 15, 2013

MIAKA 13 YA LADY JAYDEE ILIKUABALAA, MTU NYOMI

 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo jana Ijumaa June 14, 2013 kulikuwa na bonge la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hiyo wanamuziki mbali mbali walipanda jukwaani aliwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
 Wadau mbali mbali wa muziki hapa nchini wakiwemo ndani ya ukumbi  kushuhudia show hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki.
 Ndani ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama ilimradi tumsapoti Dada yetu.
 Getini mambo yako namna hii.
 Foleni bado ni ndefu na watu bado wanazidi kuingia ukumbini hapa hivi sasa.

Burudani ya Utangulizi ikiendelea.Picha Kwa Hisani ya Mroki Mroki

3 comments:

Anonymous said...

Inapendeza sana hongera sana lady jay dee unakabalika mungu azidi kukuwekea mkono wake na akutanguliw ktk,hatua azidi kuibariki kazi yako.

Anonymous said...

Hongera saaaaana dada, juhudi za jasho lako vinaonekana, hakuna wa kuzuiya riziki ya mtu hapa DUNIANI,Mola akuzidishie.

Anonymous said...

Mwenyezi Mungu akishakuwekea signature hakuna mwanadamu yeyote atakaezuia, thumbs up lady j dee