ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 15, 2013

Misa kwa Kiswahili kesho Jumapili June 16-2013

Ndugu Watanzania na Wote wapenzi wa Lugha ya Kiswahili. Ni tumaini kubwa kuwa kwa Neema za Mungu mnaendelea vyema na Familia zenu.
Kwa mara nyingine Tunawakumbusha na tunawakaribisha kushiriki Misa Takatifu kwa Kiswahili lugha ya Taifa letu na ya Kimataifa pia.
Lini?        June 16, 2013 saa 8:30 Mchana

Wapi?      St. Camillus Parish
                1600 St. Camillus Drive
                Silver Spring, MD 20903

Nani?       Mtanzania yeyote. Yeyote anayezungumza kiswahili. 

Nia:-  Kujiombea sisi tulioko ughaibuni na Familia zetu - kuombea Wababa (Ni Fathers Day), Kuliombea taifa letu amani na Kumshukuru Mungu kwa Baraka tulizojaliwa. 

Pia tutachagua Viongozi wa Jumuiya yetu. Tafadhali kama uko Tayari kutusaidia katika uongozi nipe jina lako mapema.

Naomba tutoe taarifa hii kwa wenzetu wote. 

Asanteni Sana 
Wenu Padri Evod Shao na Kamati ya Maandalizi

No comments: