Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mlezi wa Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,alipowasili katika uwanja wa Tamasha huko Mangapwani Wilaya ya Kaskazini B,Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(kulia) akiangalia Ngoma ya Mwanandege alipowasili kulifungua Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani leo huko Mangapwani Wilaya ya Kaskazini B,Unguja,(wa pili kulia) Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni
wa Mangapwani Mwinyi Jamal Ramadhan Nasib.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani Mwinyi Jamal Ramadhan
Nasib,wakiangalia Watoto waliocheza ngoma ya Kibati wakati sherehe za
Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani leo huko
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya
Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani, Mwinyi Jamal Ramadhan Nasib, wakiangalia Mchezo wa Bao la Kete wakati wa sherehe za Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani leo huko Mangapwani Wilaya ya Kaskazini B,Unguja,alipofungua Tamasha hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani Mwinyi Jamal Ramadhan Nasib, wakiangalia Akina Mama wakitwanga Mpunga wakati wa sherehe za Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani leo huko
Mangapwani Wilaya ya Kaskazini B,Unguja,alipofungua Tamasha hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani Mwinyi Jamal Ramadhan Nasib,alipovitembelea vikundi vya wajasiria mali vya Akina Mama wakati wa sherehe Tamasha hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) na Mlezi wa Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani,Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(kushoto) na Mwenyekiti wa kamati ta Tamasha Mwinyi Jamal Ramadhan Nasib, wakiangalia picha katika kikundi cha
Mangapwani Tours ambacho hujishuhulisaha na utembezaji watalii,wakati wa sherehe za ufunguzi wa Tamasha hilo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na Mlezi wa Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani,Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, (kushoto) wakimuangalia Bibi Salma Mzee Mussa wa Zingwezingwe,aliyekuwa akisuka makuti wakati wa sherehe za ufunguzi wa Tamasha hilo zilizofanyika leo katika Kijiji cha Managapwani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua mlango wa Nyumba ya kizamani ikiwa kama ishara ya Ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani,leo katika Kijiji cha Mangapwani Wilaya ya Kaskazini B Unguja Mkoa wa Kaskazini,(kushoto) Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la
Urithi wa Mila na Utamaduni wa Mangapwani Mwinyi Jamal Ramadhan Nasib. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
No comments:
Post a Comment