ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 17, 2013

Serikali yatangaza kutoa milioni 100 kwa atakayempata muhusika wa bomu Arusha.

Kufuatia tukio la mlipuko uliotokea katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi katika kata ya Soweto jiji la Arusha serikali imetoa kauli bungeni huku ikitoa ahadi ya shilingi milioni 100 kwa watu watakaofanikisha kupatikana kwa mtu aliyefanya kitendo hicho

2 comments:

Anonymous said...

Nape hawezi kuzungumza kuwa chadema ndiyo waliotega bome bila kupata idhini ya mwenyekiti wa chama chake. Wakati huo huo waziri atangaza kitita cha sh. milioni 100 kwa yeyeto atakaye saidia kukamatwa kwa mtegaji wa bomu. Kwanini hizo pesa asipewe Nape kwa sababu ameshawataja watuhumiwa? Na wale waliotajwa kwanini wasikamatwe?

Anonymous said...

hehehehehehe mto mada hapo juu umenichekesha sana. Hakika umeongea vizuri. Mie sipendi baadhi ya watu wanao kutupuka kulaumu ccm au chadema mie nataka jibu lenye uhakika na lenye ukweeli. Serikali inabidi ingurume na kukemea vikali jambo hili, maana magaidi wapo hapo hapo Arusha na si kwingine. Magaidi wanao fanya haya matukio kila kukicha wapo Tanzania si nchi nyingine. Halafu iwaje haya majanga yanatokea Arusha tu kila kukicha? something is not right here. Tunachotaka kuona ni uwajibikaji wa hali ya juuu.