ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 26, 2013

ZAWOSE KUPIGA SHOO BAGAMOYO

Msafiri Zawose
MSANII wa nyimbo za asali za utamaduni wa Kigogo ambaye anatamba ndani na nje ya Tanzania, Msafiri Zawose, anatarajia kupiga shoo ya aina yake maalum ya kuchangia kituo cha AMAP Juni 28, katika mgahawa wa PoaPoa uliopo mjini hapa.

Akizungumza jana Zawose ambaye ni mtoto wa marehemu Hukwe Zawose aliyerithi kipaji cha baba yake kwa kuendeleza utamaduni wa kabila hilo la Wagogo, alisema maandalizi ya shoo hiyo yamekamilika na tayari tiketi zimeanza kuuzwa.

"Wadau wajitokeze kwa wingi kwenye shoo yetu maalum ya kusaidia kituo cha AMAP kwa ajiri ya kuwasaidi watoto wasio jiweza kulipa ada zao za shule" alisema Zawose.

Na kuongeza kuwa mbali na burudani ya muziki pia kutakua na maonesho ya bidhaa mbalimbali sambamba na chakula cha tanzania kilichochanganya na usasa.

"Nyimbo ni kama asili yangu, kuna vibao kama Ilima, Mahera na vingine vingi"alimalizia Zawose.

kubainisha kuwa, burudani hiyo itatolewa na yeyey kwa pamoja na bendi yake hiyo ya Sauti Band.

Kwa upande wake Hannah Nelson wa walioandaa shoo hiyo alisema tiketi zinapatikana katika mgahawa huo wa Poa Poa kwa bei tsh 15,000, huku siku ya tukio Juni 28, mlangoni itakuwa tsh 20,000 ambapo kiingilio hicho kinajumuisha na chakula.

"Tiketi zinapatikana Poa Poa Restaurant, karibiuni sana katika shoo hii ambayo ni maalum kuchangia elimu" alisema Annah.

Shoo hiyo inatarajia kuanza majira ya saa 12 jioni hadi saa Sita usiku.
Kituo hicho cha AMAP (Africa Modern Art Project) kinajishughulisha na shughuli za sanaa mjini hapa na pia kinasomesha watoto wadogo.

No comments: