Matayarisho ya video ya ule wimbo ( ALL I HAVE) wa Mwanamuziki wa Hiphop ambaye ni Mtanzania aishiye jijini Chicago nchini Marekani ajulikanaye kwa jina la ARDO KING yamekamilika na video inaweza kuonekana katika mitandano mbali mbali kama youtube na website yake binafsi pamoja na facebook page yake zitakazofuata baadaye hapo chini.
Licha ya msanii huyu kufanya wimbo wa kiingereza ulioweza kukubalika sana na watu wa lugha zote, aligusia sababu na mafanikio ya kutumia lugha hiyo ni ikiwa kama kujitangaza zaidi katika mazingira yote kibiashara zaidi. "Ninaamini watanzania na watu wengi wanaotumia kiswahili wanafahamu kingereza pia,ili kueleweka katika jamii kubwa kimuziki ,niliona nifanye kitu ambacho ni universal ili hata wakazi wa hapa nchini marekani waweze kujua nafanya nini , na ulimwengu mzima pia.
Kwa namna moja au nyingine, kutumia lugha ambayo si universal inaweza kuwa na faida pia hasara yake. Lakini mimi nimeichukulia si yakimafanikio zaidi kwakuwa unajijengea uzio wa mashabiki wa aina moja tu, hususan kwa mimi niliye kati wa umati unaozungumza lugha tofauti na yangu.
Baada ya kufanikiwa kutoa wimbo huu, licha ya kuwa na nyimbo nyingine za hapo awali zilizokwisha sikika na za kiswahili, nilifanikiwa kupata show hapa chicago na airplay katika kituo kikubwa cha radio hapa nchini marekani". Ardo King ambaye wiki hii amerejea nchini Marekani akitokea bongo katika safari yake iliyolenga kuitangaza kazi yake mpya zaidi aliyoitoa katika lugha ya kiswahili na kujenga msingi wa washabiki wa nyumbani pia. "Ukiwa kama msanii, unauwezo wa kuamua ni washabiki wa aina gani unawahitaji, ukitaka mashabiki wa kichina tu ni lazima ufanye muziki wako katika lugha hiyo tu, vivyo hivyo ukitaka mashabiki wengi ni lazima utumie lugha inayoeleweka kwa wengi" aliongeza.
No comments:
Post a Comment