MBUNGE wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, amesema yupo tayari kujiuzulu ubunge, ikiwa itabainika anajihusisha biashara ya dawa za kulevya. Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kutajwa katika moja ya barua iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, baada ya mtu anayedaiwa kukamatwa China na kuwatuhumu watu kadhaa akiwamo Idd Azzan. Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu sakata hilo, alisema hatua ya kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya, ni kutotenda haki mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla.
Alisema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake, ni wazi amedhamiria kumshushia heshima na huenda akawa ana jambo limejificha.
“Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwanini hakutaka kutaja jina lake kwenye barua hiyo.
“Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa hayupo nje ya nchi, kwani katika maelezo yake anataja jina la Balozi Philip Marmo kuwa amemsaidia hali ya kuwa hivi karibuni Rais Kikwete alimteua Balozi mpya Abdulrahman Shimbo na Marmo kuwa Balozi wa Shirikisho la Ujerumani.
“Kingine naona alijaribu kuandika uongo kuweza kuaminisha jamii, kwani hata hilo jila la balozi mwanzo limetajwa jina la Bernad na kukatwa kwa wino. Ninapenda kulieleza Taifa kuwa naomba vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wa jambo hili na nikibainika ninauza dawa za kulevya nipo tayari kujiuzulu ubunge wangu.
“Kubwa haki itendeke katika kufanya uchunguzi wa jambo hili, ila ni lazima jamii na Watanzania kwa ujumla tusikubali kwa makusudi watu waichafue nchi yetu kwa chuki na fitna tu,” alisema Azzan.
Alisema kutokana na hali hiyo, anashindwa kuchukua hatua yoyote ya kufanya zaidi ya kuliandikia barua Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi dhidi ya barua hiyo kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo.
“Sijawahi kuuza dawa za kulevya na hata katika familia yangu hakuna mtu anayefanya biashara hiyo haramu. Kila mmoja anajua kuwa Idd nilikuwa Diwani wa Kata ya Magomeni, huku kazi yangu kubwa ikiwa ni biashara ya magari na daladala ambayo ninaendelea nayo hadi sasa mbali ya ubunge kama nilivyopewa heshima na wapiga kura wangu wa Kinondoni,” alisema Azzan.
MTANZANIA ilipomuuliza kuwa ni hatua gani ikibainika hakuna ukweli wa jambo hilo baada ya vyombo vya usalama kufanya uchunguzi, alisema atakachokifanya anamuachia Mungu.
“Ni ngumu kusema hatua gani nitachukua ikibainika hakuna ukweli, lakini nataka kusema kama yule aliyeandika barua hii angetaja jina lake ni wazi baada ya uchunguzi ningeweza kuomba ushauri kwa mwanasheria wangu hatua za kuchukua, lakini kwa kuwa hakutaja jina ni ngumu kuweza kuamua,” alisema Azzan.
Kwa mujibu wa taarifa zilitolewa kupitia mitandao, ziliripoti kukamatwa kwa Watanzania wawili nchini China wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya Dola milioni 3.34 za Marekani.
HABARI NA BAKARI KIMWANGA, MOSHI
CHANZO - MTANZANIA
5 comments:
Ni rahisi sana kukanusha lakini wengi wanaelewa kuwa wanaofanya biashara hiyo wana vyeo vikubwa serikalini. Hiyo barua nimeona na inaonekana ni kweli imeandikwa na huyo mtu aliye kifungoni. Mhe. Idd si rahisi mhusika akawa perfect kwenye kutaja jina la balozi, hata hivyo amejitahidi kukumbuka la pili, kumbuka jela siyo shule hivyo wafungwa hawawezi kukumbuka kwanza ni lini walitembelewa na balozi Philip Marmo na pili kama ameshabadilishwa na kuletwa balozi mwingine ukizingatia maisha ya jela ni ya stress. sioni kama ni kosa kutokukumbuka.Ukweli uliopo ni kuwa wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya si watu wa chini,ni watu matajiri na wenye vyeo, tukumbuke kuwe balozi Hassan Diria akiwa waziri wa mambo ya nje alipekuliwa huko Ujerumani lakini kila kitu kilifichwa kwa sababu ya uhuru wa kikomo uliokuwepo kwenye taifa letu. Mwisho lisemwalo lipo...inawezekana mheshimiwa Idd Azzan hahusiki lakini walio karibu yake wakawa wanahusika.
Kwanini weww unatajwa tajwa tena na watu tofauti? Hizi tuhuma hazijaanza leo na wewe unafahamu hilo. Je unaweza kutuambia kwanini jimbo lako- kinondoni ndio linaongoza na madawa ya kulevya? Je ni juhudi gani umefanya kuelimisha jamii madhara ya dawa za kulevya? Je una evidence yoyote inayoonyesha wewe kama mbunge umeshiriki directly kwenye kampeni yakutokomeza utumiaji madawa haya? Je ni nini hasa mahusiano yako na vijana hawa watumiaji wanaoshinda na wewe kwenye vijiwe na kumbi za starehe? Je unaweza kuieleza jamii kwanini
unamahusiano ya karibu na watuhumiwa wanaotajwa kufanya biashara hizi? Huoni kwamba ni wakati muafaka wakujiuzulu kupisha uchunguzi?
Jamani huyu Azzan ni zungu mbona anafahamika sana tu pale Kinondoni. Na sitoshangaa hata kama Kikwete anajuwa haya. Kujisalimisha kwake polisi siyo tatizo kwani huyu anakula na mapolisi na huenda pia anakula na kamishina wa polisi hivyo alienda pale tu ili kupata data zaidi si kujisalimisha. Iddi ni muuaji na anauza sana unga.
Nyie wote hapo juu acheni wivu wa kike!!Mie nimeisoma hio barua kiukweli imeandikwa kimajungu kumlenga kumchafua Idd Azzan...katika hio barua kuna mikanganyiko mingi sana ila ukiwa na kichwa maji utasema hio barua ni ya kweli but ni majungu yaliolekezwa kwa mh. mbunge....Kubwa ni kwann hao wengine waliotajwa ni vidagaa..mbona hakuna mapapa wenye kulingana na mbunge???No research no right to talk!
Wewe tutajie mapapa unaowajua. Huyu kataja mmoja na vidagaa. Tuviachie vyombo vya usalama. Wewe unatetea kama nani.
Post a Comment