Kiswahili hiki cha waswahili ni kama mwanaharamu huko pwani ya waswahili, masikini kimezaliwa wakati mama anajifungua akafa, kikalelewa na baba wa Kambo mwalimu Nyerere naye kwa kansa ya damu akafa.
Kiswahili aliachwa mdogo lakini mwenye afya njema akiendelea kukua, hongera kwa baba wa kambo ambaye kweli alimpenda kiswahili japo alimuua mke wake wakati akizaliwa. Kiswahili yatima ambaye sasa anabidi akue mtaani tena aitwe mtoto wa mitaani maana hata kanyaga tena ikulu wala hafla za kimataifa, labda Chissano alirejee kwenye madaraka huko nchi ya jirani Msumbiji. Hongera Chissano kukumbuka kiswahili japo TZ ulipita tu kuomba msaada wa kukomboa nchi yako, jasiri hakuacha kusahau mchango wa Kiswahili kufanikisha mambo ya Wamsumbiji.
Kwa nini tumeshindwa kutumia fursa nyingi ama zote kukistawisha kiswahili, lile baraza la kiswahili linakula tu fedha za watanzania au linafanya kazi gani??? halikumshauri hata rais kutumia fursa ya ujio wa obama kutangaza kiswahili?? au rais alikaidi?? rais si ni taasisi au huu utaasisi ni majibu ya kijanja janja kule kwa Makinda ANNE??? Hongera Kenyairways kututangazia Kiswahili duniani.
Kwa nini rais ataabike kiasi kile kuongea kiingereza wakati kiswahili kipo? hata kama rais angekuwa mzuri sana kwa kiingereza Je haikuwa fursa ya kutangaza utaifa wetu na kiswahili chetu?? hivi wajapan, wachina, warusi na waarabu wakiongea lugha zao ni kwambma hawajui kiingereza kabisa, au wanataka kuweka alama sahihi juu ya wao ni kina nani, kujitambulisha kwa dunia kuwa ni mataifa huru yenye lugha zao huru kwa matumizi yao. Kiswahili umekosa mvuto huo nyumbani na ugenini. pole haya yote yanamwisho, ama siku ukijifia au siku ukikumbukwa fedheha kilemba cha ukoko.
Kweli watanzania mmetutenda tena sana, fursa moja ikipotea mikononi na mdomoni mwa ikulu, hi hatari sana maana inaweza isije tena kwa miongo kadhaa, washauri wa rais, ikulu mnafanya nini??? mnashauri nini?? mbona imekuwa kama mnamkomesha rais? aliwakosea nini sasa mnamlipa ubaya wote huo?? si aliwaaamini mmsaidie kazi?? Kwani kiswahili kitaongewa na nani kama sio rais na ikulu ya dar??? mtoto kiswahilil kakosa nini hadi anakataliwa kwao???
Naomba serikali ifikirie tena pengine iweke mikakati kuwa rais na ikulu waongee kiswahili kwenye shughuli zote zikiwemo za kimataifa, ipo siku aibu itakuwa kubwa, narudia hii tunaona ni harufu tu, ipo siku tutaona mzoga wenyewe.
Kiswahili Kiswahili nakupenda lugha ya taifa langu.
Naomba kuwasilisha.

8 comments:
Mheshimiwa alisumbuka kidogo pale alipokuwa anajibu swali la muandishi wa habari wa Marekani kuhusu human trafficking. Kuna kipindi alikumbwa na 'tip of the tongue phenomenon' na kujikuta anajibu sehemu tu ya swali, na huo ndiyo ukawa mwisho wa press conference.
Mtoa mada, hakuna hoja nzito, rudi mezani njoo na wazo la maana.
nchi utaitangaza vipi kama lugha yako uniweka kapuni????Leaders wa Tz wanatakiwa kuongea Kiswahili ambayo lugha ya nchi,ni njia moja wapo ya kutangaza nchi yako kupita lugha yako!
Had he used Kiswahili to respond to that question, he probably would have a fear chance to prove to Americans that we are better than one man's mistake
One has to lead by examples. I praise the Prez for presenting his speech in ENGLISH. Frankly, this may motivate young Tanzanians who struggle in mastering the language in our broken education system. Equally important is to note that both Kiswahili and English are our nation official languages. Shouldn't we nourish both?
Hili ni janga la Taifa ni juzi tu pia mchekeshaji wa Tanzania Masanja Mkandamizaji amepokelewa na shada la mauwa lenye bendera ya Taifa Watanzania tunajisahau sana wala usishangae watu wengi hawatakuelewa mwandishi, kwanini TZ tunamatumizi ya Dola sana, kwanini tunapenda shule za nje, hospital za nje kuabudu wageni kupenda kuwaita watoto wetu majina ya kigeni hayo yoote ndio huzaaa magonjwa kama haya hili linaumiza sana hatiutakaa tuwe wazungu tupende vyetu
angetumia kiswahili ingependeza sana...kwa nn hatujifunzi kwa wenzetu kama wachinese,wajapanese,warussia na hata wajerumani na wafaransa???
Haya ndiyo matatizo ya kutojitegemea, utaenda kuomba Marekani kwa kutumia kiswahili? Nani atakusikiliza. La msingi ni yeye na mkewe wajifunze kiingereza. Ila akienda Rwanda na Burundi anaweza ongea Kiswahili.
Post a Comment