ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 12, 2013

JK ahadharisha wanahabari

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ametoa wito kwa waandishi wa habari kutoandika habari zenye kuchochea vurugu kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kujikuta wakiwa matatani.
Kikwete alisema hayo juzi wakati akifunga kongamano la kutafuta amani lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
“ Unaweza kuandika au kutangaza habari ya uchochezi leo, lakini vurugu zikitokea hata kama ni baada ya miaka 20 utatafutwa na kushtakiwa kwa habari hiyo,” alisema Kikwete.
Akitoa mfano, Kikwete alisema nchi za Rwanda na Kenya ni mifano hai kwa kuwa kuna waandishi wa habari ambao walishtakiwa pamoja na wanasiasa kwa uchochezi na kusababisha machafuko.
 “Nawakumbusha waandishi kuweni makini kwa habari mnazoziandika na kuzitangaza kwa kuwa mna uwezo wa kujenga na kubomoa,” alisema
Alisema vyombo vya habari,siasa  na dini vikitumiwa vibaya ni rahisi kusababisha vurugu zenye kuhatarisha maisha ya wananchi.
Alitaka TCD kuandaa kongamano kama hilo kwa ajili ya waandishi wa habari wakiwa ni wadau katika kutafuta amani.
Mwenyekiti wa TCD, James Mbatia akitoa maazimio ya kongamano hilo, alisema viongozi waandamizi wa serikali wajizuie kutumia lugha za vitisho.
Alisema pia kongamano hilo limeazimia kwamba kituo hicho kiwe karibu na vyombo vya habari na kuwahimiza kuandika habari zenye uzalendo na mshikamano wa kitaifa.
Mwananchi

4 comments:

Anonymous said...

Mh kikwete ni kiongozi safi sana maana mambo yote aliyo yasema apa nikweli nasimala yake yakwanza kuyasema uwa anaomba amani kila tamko lake ni amani kwaiyo tanzania tuna rais wa kujivunia (mambo mengine juu yake sio kweli na watu wanatangaza mabaya ya uongo kuliko mazuri ya ukweli) wasikilize wana mziki MAPACHA WA TATU bongo flava.

Anonymous said...

Tunakupenda rais wetu

Anonymous said...

I love you Mr Kikwete. Na usichokeee kukemeaaa uovu na wala usiogope chama cha upinzani baba wewe kaaaza buti tu na kama watu hawataki kufuata sharia ni kuwarusha ndani tu/jela na kama hawataki amani uzii ule ule unawasweka rumande tu. Hakuna kucheka na waovu hata kidogo wanaitia dosari nchi yeetu. Juzi mzungu kaniambia hivii "I really want to go to Tanzania but am afraid there is so much killing and also people sell drugs like Mexico it is not safe" !!!! Hiki ni kitu kilinisikitishaaa sana nusu nilie machozi the once very peaceful country is now been the talk of "not so safe" !!! Muheshimiwa Rais usicheke na kima nchi itavuna mabua aiseee. Waweke ndaniii mpaka watie akili na hakuna kutoka. Mungu ibariki Tanzania yetu.

Anonymous said...

Realy? Maneno mengi matendo hamna.