ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 12, 2013

POLISI KUPELEKA ASKARI AFRIKA YA KUSINI KUWAHOJI AGNES MASOGANGE NA MELISA EDWARD


Jeshi la Polisi litapeleka askari wake Afrika Kusini kuwahoji washiriki wa video za wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mwenzake Melisa Edward waliokamatwa nchini humo na dawa za kulevya.

Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa watawapeleka polisi kuwahoji na wanaamini wahusika watawaeleza wahusika wa mzigo huo.

Wasichana hao walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine.

“Tutawapeleka askari wetu kuwahoji, tumekwishaanza uchunguzi wa hili...wote watakaohusika katika hili tutawakamata, lakini tunakwenda polepole hatua kwa hatua kuhakikisha tunawanasa wahusika sahihi,” alisema Nzowa.

Naye Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, (JNIA), Moses Malaki alieleza kushangazwa na kiasi kikubwa kupitishwa kwenye uwanja huo licha ya kuwa wapo watu wenye dhamana ya kuangalia usalama.

“Sitaki kusema tutafanya nini, lakini ninachotaka kukwambia ni kwamba uchunguzi umeanza na suala zima tumewaachia polisi na sisi tutatoa ushirikiano kwa kila hatua watakayotutaka, lazima kukomesha hili.

“Tutaangalia nani walikuwa zamu siku hiyo,” alisema Malaki.

Mwananchi

2 comments:

Anonymous said...

NOOO!!! Kwanini Askari wa Tanzania wanaingilia hili swala wakati hawa mabinti wamepita Nyerere airport hapo Dar kama vile hawajabeba kitu na wahakusachiwa? Ningependa Police wa Tanzania wakae Tanzania wasiiiguse hii kesi waache Police wa Africa Kusini wa ngurume nao hawa mabinti yaani wawahoji na kufanya kinachotakiwa, hawa police wa Tanzania walikuwa waapi wakati kilo 150 za madawa ya kulevya yanapitishwa airport kama nguo za mwilini????? come on now. Police wa Tanzania wakishaaanza kuingilia tu that is it hawa wauza unga wataachiliwa kesho kutwa.

Anonymous said...

Inafurahisha sana kama sio kuchekesha kuhusu kutuma Polisi kutoka Tanzania waende kuwahoji watuhumiwa waliokamatwa nchi nyingine...!!! Kiukweli sijawahi kusikia UZUSHI kama huu ambao anajaribu kutafuta umaarufu wakati yeye na taaluma yake wapo nyuma mnooooo na kule wanapotaka kwenda kujidhalilisha "Eti tukawahoji watuhumiwa" ili iweje wakati wametokea hapo na kule mtaenda kuanzaje maana wao wanajua nini wanafanya na hawatumii MASABURI katika UTENDAJI... Kaa ule ofisa Godfrey Nzowa.