
Usifanye makosa kwa kujidanganya unatumia mafuta safi, mafuta yatokanayo na mimea (vegitable oils) yamekuwa si salama tena kama ambavyo tumekuwa tukiambiwa.
Ni kweli kwamba miongoni mwa vyakula bora kiafya ni pamoja na vyakula vitokanavyo na mimea, lakini mafuta yanayotengenezwa kutokana na mimea baadhi yamekuwa si salama kutokana na namna yanavyotengenezwa kuwa mafuta ya kupikia.
Ili kutengeneza na kupata mafuta meupe, mmea hupitia katika mchakato fulani kiwandani ambao kwa njia moja au nyingine hupunguza ubora na faida zinazoweza kupatikana katika mafuta yatokanayo na mmea.
Mafuta unayotumia kupikia vyakula mbalimbali, baada ya kutoka kiwandani lazima yawe bado na virutubisho ambavyo vinaweza kuhimili joto la kupikia kwa mara nyingine tena ili kuepuka kugeuka na kuzalisha kemikali za sumu kutokana na joto kali.
Hatari iliyopo ya kupikia mafuta yaliyopoteza ubora wake wakati wa kutengenezwa ni kuongeza hatari ya kubadilisha Kolestrol nzuri kuwa mbaya baada ya kutokea kitu kinachoitwa ‘oxidation’ wakati wa kupika. Mafuta mengi ya kupikia ndiyo yalivyo, licha ya kuandikwa kuwa ‘hayana kolestrol’.
YAPI NI MAFUTA BORA?
Imegundulika kuwa kwa jamii yote ya mimea, mafuta ya nazi ndiyo chaguo bora la mafuta ya kupikia, kwa sababu yenyewe huwa hayaharibiki wala kubadilika ubora wake wakati wa kupika. Aidha, mafuta ya nazi ni ya kipekee na ni mafuta yenye faida mwilini. Mafuta ya ‘Olive’ ni mazuri kiafya, lakini nayo huharibika haraka wakati wa kupika, hivyo ni mazuri kwa kumwagia juu ya saladi au mboga bila kuchemsha.
TAHADHARI
Mboga na matunda mengi hivi sasa hulimwa kwa kutumia kile kinachoitwa ‘kilimo cha kisasa’. Bahati mbaya sana, wakulima wengi hutumia mbolea zenye kamikali pamoja na madawa ya kuulia wadudu. Mbolea hizo na madawa mengine huweza kuifanya nyanya au chungwa kuwa kubwa kuliko kawaida. Unaweza kudanganyika ukadhani hayo ndiyo matunda bora, lakini nayo ni hatari sana kwa afya yako. Kula matunda na mboga zilizolimwa kwa kutumia mbolea asilia (organic farming). GPL
No comments:
Post a Comment