ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 28, 2013

`CCM ilichelewa kumchukulia hatua Mansour`

Mansour Yussuf Himid

Siku moja baada ya Mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Mansour Yussuf Himid kufukuzwa uanacahma naHalmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baadhi ya wananchi wameunga mkono uamuzi huo na kusema umechelewa kuchukuliwa na kuathiri hali ya kisiasa kwa upande wa CCM Zanzibar.

Mwinyi Issa Makame, mkaazi wa Kiembesamaki alisema Mansoor hakuwa mwanachama muaminifu wa CCM kutokana na kauli zake zilizokuwa zikikinzana na sera pamoja na ilani ya chama hicho.

Teddy Peter William, mkaazi wa Buyu alisema CCM itatenda kosa baya na la kiuonevu ikiwa wamemchukulia hatua za kididhamu yeye peke yake na kuacha wengine ambao walikuwa wakitoa maoni na msimamo kama yake.

“Nimeshangaa kusikia ni Mansour ndiye aliyetolewa kafara na wengine kuachwa,” aliongeza Teddy.

Said Shaaban, mkazi wa Mbweni Mtrekta, alisema atabaki kushngazwa kuona ni kigezo gani kilichotumika cha kumfukuza Mnsour na kuachwa kwa waziri wa zamani wa Sheria, Mzee Hassan Nassoro Moyo.

“Ameunda kamati ya maridhiano na kusema ina uwakilishi wa CCM na CUF ni uhuni wa kisasa usiovumilika, vipi aachwe na kuhukumiwa Mansoir?” alihoji Shaaban.

Katibu wa Sisa na Uenezi wa CCM wilaya ya Mjini Unguja Baraka Shamte, alisema uamuzi wa NEC ni wa kihistoria na kwamba hakutakuwa na athari yeyote kwa siasa za Zanzibar upande wa CCM.

Shangwe na vigelegele vilianza kuibuka juzi jioni baada ya habari za kufukuzwa kwa Mansour na baadhi ya wanachama wa CCM katika jimbo la Kiembesamaki walifanya karamu ya chakula kwenye matawi ya CCM.

Hata hivyo, wapo baadhi ya vijana wanaopinga kitendo cha NEC kumvua uanachama Mansoor huku wakiunga msiomamo ulioonyeshwa na Mwaklilishi huyo akiwa nje na ndani ya Baraza la Wawakilishi akiitetea Zanzibar kupata mamlaka kamili.

Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Dimani kisiwani Unguja imeunga mkono uamuzi huo.
Katibu wa Wilaya ya Dimani, Yussuf Suleiman, alisema UVCCM wilaya hiyo imepata faraja na imani kuona CCM kikifuata mkondo wa nidhamu .

Mbunge wa Dole (CCM), Sylvester Mabumba, alisema: “Hapana, hapana, niulize chochote nitatoa maoni lakini hilo waulize viongozi wa juu wa chama.”

Mbunge wa Amani (CCM), Mussa Hussein Mussa, alisema: “Sina maoni, chama kina taratibu zake kama taratibu zimefuatwa ni sawa tu, lakini mimi sijui walizungumza nini.” Mbunge wa Jang’ombe (CCM), Hussein Mussa Mzee, alisema: “No comments please (sina maoni tafadhali).”

Mwingine aliyekataa kuzungumzia suala hilo, ni Mbunge wa Mpendae (CCM) Salim Abdullah Turky
CHANZO: NIPASHE

9 comments:

Anonymous said...

ukiwa CCM lazima akili zako ziwe zimefyatuka
wanafukuzaje mwakilishi anaetoa maoni yake katika katiba na mitizamo wake?
katikba ni ya chama au ya wananchi?
CCM wana mapepo na nchi inaongozwa na watu wenye mapepo,inabidi tuyafukuze hayo mapepo 2015
nasema hivi kwani wanayoyafanya sio ya mtu mwenye akili timamu..
kwanini wasifukuze hao mafisadi,wauza unga,wauza rasilimali zetu?????????

na alichofukuzwa na kuwa na msimamo thabit kuhusu uchimbaji wa mafuta japo kuwa hawatoweza kukisema mbele ya hadhara ya wananchi walala hoi

Anonymous said...

Umeonaee..Magamba hata sijui nchi yetu yanaipeleka wapi. Wakosaji hawaguswi ila watenda haki na wenye maoni tofauti na wao wanaadhibiwa kipigo cha mbwa mwizi....wamefanya kufikiria maana ya siasa na serikali ktk uharisia tofauti, I mean serikali na siasa vionekane kama ni tasinia ya wahuni, wezi na genge la mafia

Anonymous said...

Nape Nnauye anasemaje juu ya hili? Maana amewahi kusema kuwa wanachama wa CCM ambao pia ni viongozi wa kuchaguliwa na wananchi uamuzi wowote wa kuwavua uanachama ni lazima uridhiwe na kamati kuu(tukirejea sakata la mameya wa Bukoba), huyu nae si wakundi hilo?
Ama wanachama wa CCM Zanzibar na CCM bara wanahadhi tofauti???

Anonymous said...

Sasa muziki umeanza, namsihi awe makini afanye yafuatayo:-
1. Muda wote avae helmet kuepuka kuwagiwa tindikali.
2. Atembee muda wote na pain killer kwani muda wowote anaweza kung'olewa kucha na meno.

Anonymous said...

Sarakasi hizi.

Hivi wale madiwani 7 kanda ya ziwa walivuliwa halafu wakavalishwa? au?

Anonymous said...

Teh teh madiwani wa bukoba wamepewa uanachama wao, wazanzibar wamenyimwa nafasi! Kweli ccm ni kaburi la wazanzibar!

Anonymous said...

KATIBA ya ZNZ iliyofanyiwa marekebisho makubwa mwaka 2011 INAKATAZA MWAKILISHI AU SHEHA kupoteza nyadhifa yake kwa sababu tu eti chama chake kimemfukuza!Katiba inasema MWAKILISHI/SHEHA atapoteza tu madaraka yake kwa sababu MWENYEWE KAJIONDOA kwenye chama!

Mansoor ATAENDELEA KUWA MWAKILISHI WA kiembe samaki hadi uchaguzi mkuu wa 2015!Lissu Antipas Tundu alikuwa right aliposema kuwa MUUNGANO wa TZ umevunjika siku nyingi kilichobaki ni ulaji tu!

ZNZ ina mamlaka yake kamili ndani ya CCM na sheria za CCM za Bara HAZIFANYI KAZI Zanzibar!

Anonymous said...

Hao huwa hawafukuzani. Utasikia wamepeana onyo la kishkaji then msala unaisha. Si unacheki walichokifanya kule Bukoba? Ni chama kilichokaa kishkaji zaidi.
Wanawadanganya walalahoi wasio jua mambo yanavyokwenda

Anonymous said...

hongereni, swali ni wangapi wenye msimamo huo mtawafukuza? je mtakirudisha kiti hicho