
Aidha, NEC imethibitisha kupokea barua za madiwani hao za kukata rufaa walizoziwalisha taifa, wakipinga uamuzi uliofanywa na halmashauri kuu ya mkoa, kwa msingi wa kukiukwa kwa utaratibu katika kufikia uamuzi huo.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipozungumza na waandishi wa habari.
Alisema kwa mujibu wa utaratibu wa chama wa kutoa adhabu, halmashauri ya mkoa ilikosea kufikia maamuzi hayo ya kuwafutia dhamana ya CCM na hivyo kuwavua udiwani.
“Kuna utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola, hasa wabunge na madiwani, kwamba uamuzi wa mkoa unakuwa siyo wa mwisho, bali ukishafikiwa, unapaswa kupata Baraka za kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa (CC), ndipo uweze kutekelezwa,” alisema.
Alisema kwa hali hiyo, madiwani waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao za kuwatumikia wananchi kama kawaida, wakisubiri kikao cha CC, kitakachoketi Agosti 23 mwaka huu, ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa mkoa.
Juzi, CCM Mkoa wa Kagera kupitia kwa katibu wa chama hicho, Avelin Mushi, ilitoa taarifa ya kuwatimua madiwani wake, kufuatia mgogoro wa uongozi wa siku nyingi katika Manispaa ya Bukoba, mkoani humo.
Madiwani waliokumbwa na kadhia hiyo, ni Yusuph Ngaiza (Kashai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bukoba; Samuel Ruhangisa (Kitendagulo);Murungi Kichwabuta (Viti maalumu) na Deusdedith Mutakyawa (Nyanga).
Wengine ni Richard Gaspal (Miembeni); Alexander Ngalinda (Buhembe) ambaye pia ni Makamu Meya; Dauda Kalumuna (Ijuganyondo) na Robert Katunzi wa Kata ya Hamugembe.
CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Suala la kujivua gamba limeishia wapi muheshimiwa Nape. Au ndiyo kusema watanzania tuna kumbukumbu fupi?
Post a Comment