UkiwaNewYork City huwezi kuboreka kwani kuna mambo mengi tu ya kukufanya uwe mchakamchaka kama kibaraka yakufurahisha na kukuachia kumbukumbu kwani hakuna kama New York city. Hapa ni sehemu ya kupandia boat la kukupeleka Statue of Liberty.
Boat hilo likiwafuata watu baada ya kuwashusha huko Statue of Liberty
Hapa ndiyo watu hushushwa na kulizunguka eneo hili kwa kupiga picha na kujua historia ya sehemu hii muhimu sana .
Hawa ni watu wamevaa kwa mfano wa sanamu hilo kama unavyo ona unaweza kupiga nao picha kwa kuwalipa kitu kidogo ili na wao wasikae bure hapo juani. Mambo ya New York hayo.
New York pia ni makao makuu ya Umoja wa mataifa na jengo hili ndiyo makao makuu ya umoja huo wa mataifa wenye nguvu dunia. Viongozi duniani kote kila mwaka hukutana hapa na kujadiri mstakabali wa dunia unavyooenda. Kama unavyoona kuna bendera ya Tanzania katikati ya bendera za mataifa mawili makubwa dunia jibu unalo hapo.
Hapa ni geti kuu la kuingilia kwenye mjengo huo wa umoja wa mataifa New York City.
Hapa ni Time Square New York hiyo hiyo jamaa akitoa pesa hili apate ukodak na dada huyo mwenye nguo za faragha.
Ameshalipia ukodak na dada anaweka pesa yake kipindoni.
Pozi la ukodak baada ya kunywa dollar yake, mambo haya ni New York mchana kweupe na jamaa kashikishwa kipango kinachoonyesha wapi picha hiyo imepigwa.
Hii ndiyo New York City jiji la wasilo lala
New York kuna mabasi makubwa kama haya unalipia na kuzungushwa uku sehemu mbalimbali Manhattan New York..
Baskeli nazo zipo unanunua kadi maalum na kisha unachanja na baskeli inatoka unazunguka nayo mtaani hadi uchoke. Hapa mdau Maro akipata ukodak na huku akisema akirudi bongo na yeye atafungua mradi kama huu sasa swali wakodishaji tarudisha???
Usije ukafikiria kuwa ni sanamu hao ni watu wako kazini ukipita dondosha ulichonacho nyumbani mama watoto maji ya ugali yapo jikoni baba kazini akrudi na pesa ya mboga maisha yana songa siku imepita yote ni NYC.
Mchakamchaka ndani ya New York ni burudani tosha kama unavyoona chunguza picha na utaona tu mambo ya kukufanya ushangae ukiwa New York hasa kipindi kama hiki cha jua.
Jamaa nae akitoa pesa yake ili apate ukodak na huyo dada mwenye vinguo vya chumbani. na mwili mzima akiwa amepaka rangi ili kupunguza ukali wa kivazi chake. Hii yote anafanya ili hapate pesa na kuendesha maisha yake ya kila siku ndani ya New York City.
Kapozi na mabegi yake mrembo pembeni huku anapata ukodak wa kumbukumbu akiwa new York.
Ukitaka kupiga picha toa kidogo ulichonacho
Camera ya Vijimambo ilitoboka kidogo ikapata pozi kama hiyo na kupata ukodak watu peopleeeee!!
Karibu New York City nyumbani kwa Umoja wa Mataifa na jiji la wasilo lala mchana usiku kucha
No comments:
Post a Comment