ASKARI wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini DR Congo (MUNUSCO), wakiongozwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vimefanya shambulizi la nguvu katika eneo la Kibati (Nyirangongo Territory, Goma, Eastern DRC), eneo hilo ndiyo iliyokuwa ngome kuu ya waasi wa M23
Shambulio hilo kubwa na la kwanza kufanywa na vikosi vya Umoja wa Mataifa limekuja siku moja, baada ya Askari wa JWTZ kuuawa na waasi wa M23 katika shambulio lao la juzi wakati vikosi vya UN vilipokuwa katika ukaguzi wa maeneo yenye usalama katika mji wa Goma.
Askari huyo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ Khatibu Mshindo aliuawa kwa kupigwa bomu juzi na waasi wa M23 kwenye Mji wa Goma ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano makali.
Mshindo aliuawa baada ya mapigano makali yanayoendelea katika Mji wa Goma, ambapo ilielezwa kwamba Askari wa M23 waliwazidi ujanja majeshi ya Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini Congo.Wakati Mshindo ambaye alikuwa miongoni mwa askari wa Tanzania wanaounda Jeshi la Umoja wa Mataifa akifikwa na mauti, wapiganaji wengine 10 walijeruhiwa.
Waasi wa M23 waliokuwa Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema kuwa watasitisha mapigano, kufuatia makabiliano makali na wanajeshi wa serikali wanaoungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.
Wakati M23 wakidai kwamba watasitisha mapigano hayo, taarifa zaidi zinaeleza kwamba Majeshi ya UN yanayo ongozwa namajeshi ya Tanzania yamefanya mashambulizi makali ya mizinga pamoja na Askari wa Miguu wakipanda milima na kuwasambaratisha waasi wa M23 na kuteka ngome yao.
No comments:
Post a Comment