ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 28, 2013

MBUNGE ALIYEVULIWA UANACHAMA WA CCM MANSOOR YUSSUF HIMID AZUNGUMZA NA RADIO UJERUMANI (DW)

Mansoor Yussuf Himid

Idhaa ya Kiswahili ya radio ya Ujerumani,jana katika kipindi chake cha mchana (saa za Afrika Mashariki) imetangaza mahojiano mafupi ambayo yalifanywa na mtangazaji wa redio hiyo na aliyekuwa Mbunge wa Kiembesamaki, Mjini Magharib, Unguja aliyevuliwa uanachama na hivyo kupoteza nyadhifa zake kichama na Kiserikali, ndugu Mansoor Yussuf Himid na kumwuliza maswali kadhaa kuhusiana na kilichotokea kwenye uamuzi wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinzuzi kilichofanyika huko Dodoma na kutangazwa kwenye vyombo vya habari hapo jana.

Hapa ninanukuu nilichokisikia.

Mwandishi wa DW: Umeuchukulia vipi uamuzi huo?

Mansoor Yussuf Himid: Nimepata taarifa hizo za Chama Cha Mapinduzi, chama changu kunivua uanachama. Niseme kwamba namshukuru Mwenyezi Mungu na nimepokea kwa hatua hii kwa namna ilivyotoka. 

Mwandishi: Kwa maana chama ambacho umekulia humo na mzee wako Yussuf Himid alikuwa mwasisi leo hii haumo?

Himid: Ndiyo wenzangu wameashaamua hivyo. Basi hatua hii yatosha hayo.

Mwandishi: Na zipi fikira zako zilizokujia haraka haraka kichwani baada ya uamuzi huu?

Himid: Nimemshukuru Mwenyezi Mungu

Mwandishi: Umefika ukingoni katika uwanja wa siasa?

Himid: Bado ni mapema mno na sikuwa na dhamira ya kuzungumza lakini wewe mwenzangu umeniuliza na

unanipigia simu hii siku ya tatu ya nne mfululizo, nikasema nikupe heshima angalao basi niseme mawili matatu, na kwa sasa yatosha. Lalini wakati utafika nitakapokuwa nimejihahikishia mimi mwenyewe, kwamba saa niko tayari kuzungumza, nitasema hayo machache ambayo ninayo na ninadhani yanafaa kuzungumzwa.

Mwandishi: Kuna tuhuma kadhaa zimetajwa ambazo zimesababisha pengine uondolewe chamani, hizi unazizungumziaje?

Himid: Ndugu yangu, nimezisikia hizo tuhuma. Na kama nilivyokwambia  mwanzo, unajua wanasema “anayekutukana hakuchagulii tusi,” sasa madamu zimeletwa hizo tuhuma na wenzangu wameziona za msingi kujadiliwa na ndiyo za msingi wa mimi kuvuliwa uanachama, kama nilivyokwambia namshukuru mwenyezi mungu.

Mwandishi: Kwa safari hii, kwa yale yote yaliyosemwa bila shaka wasikilizaji wangependa kujua --kuna ukweli katika hili, kuna uoneaji katika hili-- wewe binafsi unasemaje?

Himid: Hatua hii bado ni ya  mapema mno.

Mwandishi: Unazungumziaje demokrasia ndani ya Chama Cha Mapinduzi?

Himid: Nikiwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nikiwa Mzanzibari kwenye huu utaratibu unaoendelea wa kutafuta hiyo katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitaendelea kuzungumza yale amba yo mimi ninayaamini.

Mwandishi: Kwa kutukumbusha tu, yapi ya msingi ambayo wewe unaamini?

Himid: Mimi ninaamini huwezi kuwa na katiba ya maana, ya msingi inayoridhiwa na wingi wa watu ikiwa hakuna uhuru wa watu kujieleza. Ni udaganyifu na upotoshaji mkubwa. Huwezi kuwa na Katiba ya maana, na inayoandikwa na watu wa maana, na nchi ya maana ikiwa hakuna fursa ya watu kueleza yale waliyokuwa nayo ili hatimaye maamuzi yawe yale ambayo yaliridhiwa na wengi. Kwa hivyo naendelea kusema hilo niliendelea kuliamini hilo huko, ninaendelea kuliamini hilo hivi sasa. Na ikiwa hilo halijapatikana basi nafikiri tunaendelea kucheza mchezo ambao hauna mwelekeo.

Mwandishi: Una wasiwasi kwamba pengine rasimu ya Katiba Mpya haitazaa matunda mema ya kuleta Katiba iliyo bora kwa maslahi ya wote?

Himid: Matumaini ya Wazanzibari kwa hapa tulipofika hayazuilka. Wakati wake utafika. Limezama katika nafsi na nyoyo za Wazanzibari na wanachokitaka  ni very simple, wanataka haki hayo ya kusikilizwa, wanataka haki yao na wao kuwa na nafasi yenye heshima iliyo kuwa ya haki na ya  usawa ndani ya Muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwandishi: Hili ni moja kati ya ya sababu ambazo pengine zimesababisha uondolewe katika Chama, kwa nini umeshindwa kutumia majukwaa ama mikutano ya chama kufanikisha azma yako?

Himid: Looh, ndugu yangu kama nilivyokwambia wazi, sikuwa tayari kuzungumza hivi ghafla.

Yalikomea hapo mazungumzo hayo.

9 comments:

Anonymous said...

ukiwa CCM lazima akili zako ziwe zimefyatuka
wanafukuzaje mwakilishi anaetoa maoni yake katika katiba na mitizamo wake?
katikba ni ya chama au ya wananchi?
CCM wana mapepo na nchi inaongozwa na watu wenye mapepo,inabidi tuyafukuze hayo mapepo 2015
nasema hivi kwani wanayoyafanya sio ya mtu mwenye akili timamu..
kwanini wasifukuze hao mafisadi,wauza unga,wauza rasilimali zetu?????????

na alichofukuzwa ni kuwa na msimamo dhabit wa kuhusu uchimbaji wa mafuta japokuwa hawajakisema

Anonymous said...

Umeonaee..Magamba hata sijui nchi yetu yanaipeleka wapi. Wakosaji hawaguswi ila watenda haki na wenye maoni tofauti na wao wanaadhibiwa kipigo cha mbwa mwizi....wamefanya kufikiria maana ya siasa na serikali ktk uharisia tofauti, I mean serikali na siasa vionekane kama ni tasinia ya wahuni, wezi na genge la mafia

Anonymous said...

Nape Nnauye anasemaje juu ya hili? Maana amewahi kusema kuwa wanachama wa CCM ambao pia ni viongozi wa kuchaguliwa na wananchi uamuzi wowote wa kuwavua uanachama ni lazima uridhiwe na kamati kuu(tukirejea sakata la mameya wa Bukoba), huyu nae si wakundi hilo?
Ama wanachama wa CCM Zanzibar na CCM bara wanahadhi tofauti???

Anonymous said...

Sasa muziki umeanza, namsihi awe makini afanye yafuatayo:-
1. Muda wote avae helmet kuepuka kuwagiwa tindikali.
2. Atembee muda wote na pain killer kwani muda wowote anaweza kung'olewa kucha na meno.

Anonymous said...

Sarakasi hizi.

Hivi wale madiwani 7 kanda ya ziwa walivuliwa halafu wakavalishwa? au?

Anonymous said...

Teh teh madiwani wa bukoba wamepewa uanachama wao, wazanzibar wamenyimwa nafasi! Kweli ccm ni kaburi la wazanzibar!

Anonymous said...

KATIBA ya ZNZ iliyofanyiwa marekebisho makubwa mwaka 2011 INAKATAZA MWAKILISHI AU SHEHA kupoteza nyadhifa yake kwa sababu tu eti chama chake kimemfukuza!Katiba inasema MWAKILISHI/SHEHA atapoteza tu madaraka yake kwa sababu MWENYEWE KAJIONDOA kwenye chama!

Mansoor ATAENDELEA KUWA MWAKILISHI WA kiembe samaki hadi uchaguzi mkuu wa 2015!Lissu Antipas Tundu alikuwa right aliposema kuwa MUUNGANO wa TZ umevunjika siku nyingi kilichobaki ni ulaji tu!

ZNZ ina mamlaka yake kamili ndani ya CCM na sheria za CCM za Bara HAZIFANYI KAZI Zanzibar!

Anonymous said...

Hao huwa hawafukuzani. Utasikia wamepeana onyo la kishkaji then msala unaisha. Si unacheki walichokifanya kule Bukoba? Ni chama kilichokaa kishkaji zaidi

wanawadanganya walala hoi wasiojua mambo yanavyokwenda na kujijia hapa kwenye blog kujisomea somea na kuishia mitini

Anonymous said...

hongereni, swali ni wangapi wenye msimamo huo mtawafukuza? je mtakirudisha kiti hicho