Mwenyekiti wa mtaa Noel Mseven akiufunua mwili wa marehemu watu waweze kuutambua.
Mwanamke huyo ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka alikuwa amevaa Blauzi nyeusi yenye madoa meupe, viatu vyenye urembo wa silva, mnene kiasi, mweusi na mwenye nywele ndefu.
Mwili wa Mwanamke huyo amegunguliwa leo majira ya saa sita Mchana baada ya watu waliokuwa wanachimba kaburi kuuona mwili huo pembeni ya eneo hilo na kutoa taarifa Polisi.
Wananchi wakisaidiana na Polisi kuubeba mwili wa marehemu.
Kwa mujibu wa majirani wanaoishi eneo la makaburi hayo, tukio hilo linakisiwa kutokea usiku wa kuamkia jana huku baadhi ya kina mama wakisema kuwa walisikia sauti ya mwanamke akipiga mayowe katika eneo la mnadani.Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo Kaskazini Noel Mseven amesema amepata taarifa kutoka kwa wananchi na baada ya kufika katika eneo hilo walibaini kuwa sehemu za siri za mwanamke huyo ziliingiziwa kitu chenye ncha kali.
Jeshi la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku Mrakibu msaidizi wa Polisi Aziz Mayunga akitoa wito kwa wananchi kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kuutambua mwili huo.
Tunaomba radhi kwa picha hii ni kwamba mpaka sasa hivi mwili wa marehemu haujatambuliwa tunajaribu kuuonyesha ili kama kuna mtu yeyote anayemfahamu ajitokeze.
1 comment:
Binaadam tunakwenda wapi jamani!
Post a Comment