ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 26, 2013

SIKU YA POLISI ILIVYOADHIMISHWA LEO MKOANI MOROGORO

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustini Shilogile akitoa taarifa kuhusu maadhimisho ya miaka 94 ya Jeshi la Polisi Nchini iliyoadhimishwa jana.Ambapo Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro walifanya usafi kwenye Kambi ya kulea wazee na wasiojiweza ya Funga funga na Kutoa msaada kwa wazee hao pamoja na watoto yatima wa kituo cha Mgolole.
Mwenyeki wa wazee akitoa Neno la shukrani wakati wa ugeni huo wa polisi walivyotembelea kambi yao ya wazee na wasiojiweza wa funga funga Mkoa Morogoro 
Bibi aliyekuwa kwenye kambi ya wazee wa Funga funga anakadiriwa kuwa na miaka 105.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustini Shilogile akiwa Na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro Japhet Kibona wakifanya usafi katika kambi ya kulea wazee na wasiojiweza ya Funga funga

No comments: