Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala mbalimbali likiwemo pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la kumvua uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid (pichani), Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kiembesamaki.
Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf Himid ni pamoja na:-
1. Kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.
2. Kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa CCM.
3. Kuikana Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.
Baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu Mansoor Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa CCM.
Imetolewa na:
Nape Moses Nnauye,
KATIBU
WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
26/08/2013

2 comments:
USIHUZUNIKE SANA MUONE MAALIM HARAKA ATATATUA TATIZO HILO.
MAMBO MADOGO SANA HAYO.
pole kijana, naona hili tukio pengine litakupa darasa. siasa haikufai sasa katafute chuo usome au ukafanye biashara. wako wengi kama wewe wanaingizwa katika siasa kama kina Prof Lipumba na wengineo kasha wanapwaya na wasijue wanafanya nini. nadhani sasa utajifunza kwa makosa yako, madaraka, ubadhirifu na baadae mnatafuta namna ya kuziba mashimo mlioyachimba, UZANZIBARI HALISI hiyo nayo haikutosha kukuokoa, wengine walipokuwa wakiyataka madaraka waliwanyenyekea wabara na kuusifia na kuulinda muungano na mfumo wake huu huu uliopo, hawakuhoji hati za mikataba ziko wapi wakiwa marais. sasa hawapo wanahoji hati za muungano SHAME ON YOU!! wanafiki wakubwa. nnacho kiona mimi Tanzania yetu au Zanzibar yetu bado haijapata viongozi wa kuongoza bali wengi wao wanataka madaraka na kufanya mambo ya ajabu ya kuwachanganya wananchi wengi wao hawajui washike lipi. serikali mbili, moja, tatu, tupumue, mkataba au vunja kabisaaa!! Mwisho wa haya yote na tafrani hii maneno ya Nyerere yatathibitika, ukivunjika huu uliopo sasa utavunjika wa wabara na wa hao wa visiwani pia dalili za kutosha zipo kwani hivyo vikao vilivyojadili jadili siasa za Zanzibar wakubwa wengine walishasema bora wapemba na waunguja wagawane mbaooooo. salaaaale wengine hawautaki uwo ukweli, na bara nako sijui lakini wanadini washachokana
Post a Comment