ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 17, 2013

Watanzania Tunajifunza Nini Kutoka Misri?


Yapata karibia miezi miwil hivi tumekuwa tukishuhudia kuchafuka kwa nchi muhimu sana katika bara letu zuri la Afrika. Kupitia vyombo mbali mbali vya habari, televisheni, redio, magazeti , mitandao ya kijamii na tovuti mbali mbali. Kwa watu ambao tumepata bahati ya kuitembelea Misri na kuona inakoelekea kwa sasa inaudhunisha sana. Chokochoko hizo zilizoanza kwa jina la demokrasia sasa zimepelekea watu elfu moja kupoteza maisha mpaka sasa.
Nafasi ya Marekani katika mvulugiko unaoshuhudiwa nchi Misri. Wote tunatambua kwamba Misri ndio nchi ya pili kupokea mamilioni ya pesa ikidaiwa ni msaada kuoka Marekani. Nchi ya kwanza kupokea pesa kutoka bajeti ya Marekani ni Israel. Kati ya pesa nyingi zitolewazo na Marekani kwa Misri asilimia tisini ya pesa hizo uelekezwa kwenye shughuli za kijeshi. Ukijiuliza kwanini sio shule au hospitalini, jibu hakuna
Baada ya mapinduzi yaliyofanywa na jeshi la Misri likidai ni kwa maslahi ya wananchi, kwa kumwondosha rais aliyechaguliwa kwa kura za wanachi wa Misri. Marekani nchi ipendayo demokrasia imegoma mpaka kesho kusema kwamba ni mapinduzi ya kijeshi. Rais Mohamed Morsi ambaye alipigiwa kura na Wamisri kupitia chama cha Muslim Brotherhood amesalia gerezani mpaka kesho.
Nchi za Magharibi zikiongozwa na baba yao mkubwa Marekani zimekaa kimya mpaka apo jana Rais Barack Obama aliposema kwamba Marekani inasitisha mazoezi ya kijeshi na Misri. Wamisri wameedelea kuuwawa, kuteseka, kusalia majiani, uchumi wa Misri umeendelea kuporomoka na mahusiano kati ya watu wa dini mbali mbali nchini Misri yameendelea kuwa mabaya zaidi.

Tukirudi kwenye historia tukaangaza kinachotokea Misri wengi tunaweza kusema ni mpango mzima ulioandaliwa kwa muda mrefu na nchi za Magharibi lakini Wamisri wao hawakuweza kuangaza macho mapema. Lugha nzuri ya Kimagharibi yenye kuongelea Demokrasia ikiwa imefungwa na maboksi mazuri ya misaada iliwapumbaza Wamisri.
Nasema hivyo kwa mfano mdogo sana wa Watawala wa Misri kwa sasa. Katika uchaguzi ulioitwa wa kidemokrasia wagombea maarufu wawili ni wasomi waliosomea hapa Marekani. Mohamed Morsi amesoma University of Southern Calfornia, na Mohamed El Baradei alisomea New York University. Wote wanaelewa ni kitu gani unapoongelea demokrasia kadiri ya Wamarekani au nchi za magharibi.  
Mohamed Morsi kwa kujiunga na Muslim Brotherhood kwa macho na mtizamo wa Wamarekani alikuwa amejichafua, na mara moja Wamarekani na nchi za Magharibi wakayaelekeza macho yao kwa Mohamed El Baradei na kuweka matumaini kwamba atashinda. Lakini mategemea yao yaligonga mwamba, baada ya Mohamed Morsi kukamata dola la Misri. Choko choko ilianzia hapo.
Wakaja na sababu ambayo si ya kweli na kusema kwamba kwa kuwa Muslim Brotherhood wameshinda Madheebu ya Kikristo yatakuwa kwenye shida ya kuwindwa na Waislam. Waliendelea kulazimisha sababu hiyo na kuiaminisha dunia nzima kwamba ni kweli. Jambo ambalo alikuwa na mashiko. Kwani Waislamu na Wakristo ndani ya Misri wameishi pamoja toka enzi kabla hata hivyo vijisenti vya Marekani avijaanza kupelekwa Misri
Kupinduliwa kwa Mohamed Morsi  ilikuwa ni matokeo ya visingizio vya Kimagharibi ambavyo daima utupeleka pabaya. Tamaa za Waafrika hasa wachache kwa kukubali vijisenti na kuuza haki za walio wengi ndio matokeo tuyaonayo Misri leo.
TANZANIA JE? Ndugu zangu watanzania tuna mengi ya kujifunza kutoka Misri tena kwa umakini zaidi. Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alisema “Ubepari ni Unyama” mpaka kesho kuna watu wanaendelea kumlaumu kwa kauli hii. Lakini ningewaomba wale ambao wanamlaumu wachukue muda kufikiria hali ya Misri na Zimbabwe.
Hivi karibuni Watanzania tulipata bahati ya kutembelewa na Marais watatu wa Marekani tukianza na Rais Barack Obama, na marais wastaafu George Bush na Bill Clinton. Kwetu ilikuwa furaha kwani Marekani ni nchi kubwa na ni muhimu sana kwetu kuwa na mahusiano mazuri na Marekani.
Lakini swali moja ambalo tunajiuliza kimya kimya bila kupaza sauti, NI  KWANINI WAMECHAGUA TANZANIA? Hapo tutatofautiana sana kwa majibu kwani wengine twaeza kuwa na mitizamo tofauti katika suala hili. Kuna wanaosema kwa kuwa Tanzania ni kisima cha amani, wengine wanasema Tanzania tumekuwa mstari wa mbele katika utetezi wa haki za binadamu. Majibu yote yanavutia na ni ya kweli kwa kiasi fulani
Sisi tuliopata bahati ya kuishi nchii hii (Marekani) twaweza kuwa na majibu mazuri zaidi kuliko labda wale wanaoishi nyumbani. Ndugu zangu hapa Marekani kuna omba omba, watu wasiokuwa na makazi (homeless), ulala majiani, shule zinafungwa kwa sababu ya kukosa pesa, watu wanajipanga kwenye msululu wa kutibiwa kwa sababu hawana bima ya maisha, watu wanajipanga kupata chakula cha msaada (food pantry)  na mengi mengineyo.
Lakini cha kushangaza nyumbani tunapewa Mamilioni ya pesa ya msaada. Na bila kujiuliza tunapiga makofi na kuwachezea ngoma. Hayo hayo mamilioni ndio yanayoimaliza Misri kwa kivuli cha demokrasia. Najua sisi tulio wengi upenda furaha ya muda mfupi na saa nyingine ni vigumu kwetu kuangaza mbali na kuzifanya hakili zetu zifikirie mbali zaidi zaidi ya leo.
Ndugu zangu Wamisri waliishi pamoja hata kabla ya Taifa la Marekani kuzaliwa,  leo hii wanaambiwa Waislam wanawachukia Wakristo, na wao kwa sababu wameishakubali mapesa yao inabidi wakubali. Kwahiyo na Wamisri wamekubali kwamba ndio kuna chuki kati yao. Na bunge la Marekani linaongelea kuwapa ifadhi Wakristo wanaoteseka huko Misri. Jamani chuki hiyo imezaliwa siku mbili hizi?
Tanzania je? Tunayoyaona Misri Tanzania yameanza, chokochoko ndogo ndogo za kisingizio cha dini. Tunasikia nchi inaongozwa na mfumo Kikristo, achinje nani? Polisi wanaonea dini fulani. Taratibu mambo haya tunayaona na kuyasoma kwenye vyombo vyetu vya habari. Siwezi kusema yameletwa na Marekani lakini kama Mwl. Nyerere alisema ukweli kwamba ‘Ubepari ni Unyama’ na kama mabepari wameishavamia nchi yetu basi hapo kuna kitu. Inawezekana wameishasambaza unyama wao.
Watupumbaze kama walivyowapumbaza Waafrika Kusini kwa kuwapa Uhuru hewa na mpaka leo Waafrika kusini asili ni masikini wa kutupwa ingawa uchumi wan chi huko juu. Na Sisi watupumbaze wakituacha tukigomabana kuhusu Nani Achinje, Nani Bora kati ya Mkristo na Mwislam, wakati huo huo maliasili yetu ikiamia katika nchi zao za Magharibi.
Watanzania wenzangu lazima kufungua macho yote mawili bila kufumba, lazima kuamuka na kujivunza kutoka kwa wenzetu sio kila kingaacho ni zahabu. Lengo letu ni kuhakikisha kila mtoto wa Mtanzania anakwenda shule, anatibiwa na anapata lishe. Kwamba ni Mwislam au Mkristo alijawahi kuwa tatizo letu, kwa nini liwe leo. Kuna kajiswali muhimu hapo.
Ndugu zangu wakati wenzetu Wachina na Wahindi wanasambaza Mainjinia duniani kote Sisi kazi yetu ni kusambaza wataalamu wa kuuza Madawa ya Kulevya!!!!! Lazima tujiulize na kuanza kujipanga, tamaa ya wachache itatutumbukiza kwenye haya tuyaonayo Misri.
Ndugu zangu Waislamu na Wakristo kwa pamoja lazima kupaza sauti na kusema kwa pamoja kwamba hili hapana, la sivyo Umisri unatunyemelea.

Yangu ni hayo-Karibu kwa maoni.  

3 comments:

Anonymous said...

umemaliza yote ndugu mwandishi ni kweli yote ulioyaandika lakini watanzania wenzangu watakuelewa?Mungu ibariki Africa Mungu bariki TANZANIA NA VIONGOZI WAKE UWAPE UFAHAMU YA KUONGOZA WATU NA SERA NZURI

Anonymous said...

OMG Jesus Christ. I`m crying for your message, because everything is true. And I`m saying as a Christian person and I do live in USA.
My Brother/ Sister Sometimes I just wish people they could see the truth and I do pray for that. Tanzania is a very good country and I love it with all my heart, I`m so proud to be Tanzanian because I feel like I`m unique different unlike other country. Its true the way country it is now not so good like it used to be . I blame to the all Tanzanian leaders who are very selfish,ungrateful who don`t care their people and middle class at all. They promised and don't keep their promises.
They do have everything they wanted but stills refuse to hear Middle class voice. Sometimes I wish God to eliminate all leaders who don't do fair to their own people. Now these days if you are middle class , poor need help you cant get help. But if you have a popular name and need help you will see all leaders will help because you are rich like them, hello what about us. I'm just praying to God through Jesus Christ to hear Middle Class`s tears, Lord we need your Hand oh Jesus come and wipe our tears away . We are so tired oh Lord with Evil doing from selfish Leaders. Jesus please come to take your Holly Church in Jesus Name Amen.

Anonymous said...

Tanzania inabidi tuchange true demokrasia ya ukweli siyo mambo ya kurithi njenje au a few always in power abd never retire. Rushwa za kijinga hazitufikisha popote zaidi ya umaskini kiakili...time tanzania iwe for tanzanians siyo watu weingine using tz passports na kubba madawa au upuuzi mwingine...and pay the real teachers, police and mostly the doctors