
Yapata karibia miezi
miwil hivi tumekuwa tukishuhudia kuchafuka kwa nchi muhimu sana katika bara
letu zuri la Afrika. Kupitia vyombo mbali mbali vya habari, televisheni, redio,
magazeti , mitandao ya kijamii na tovuti mbali mbali. Kwa watu ambao tumepata
bahati ya kuitembelea Misri na kuona inakoelekea kwa sasa inaudhunisha sana.
Chokochoko hizo zilizoanza kwa jina la demokrasia sasa zimepelekea watu elfu
moja kupoteza maisha mpaka sasa.
Nafasi ya Marekani
katika mvulugiko unaoshuhudiwa nchi Misri. Wote tunatambua kwamba Misri ndio
nchi ya pili kupokea mamilioni ya pesa ikidaiwa ni msaada kuoka Marekani. Nchi
ya kwanza kupokea pesa kutoka bajeti ya Marekani ni Israel. Kati ya pesa nyingi
zitolewazo na Marekani kwa Misri asilimia tisini ya pesa hizo uelekezwa kwenye
shughuli za kijeshi. Ukijiuliza kwanini sio shule au hospitalini, jibu hakuna
Baada ya mapinduzi
yaliyofanywa na jeshi la Misri likidai ni kwa maslahi ya wananchi, kwa
kumwondosha rais aliyechaguliwa kwa kura za wanachi wa Misri. Marekani nchi
ipendayo demokrasia imegoma mpaka kesho kusema kwamba ni mapinduzi ya kijeshi.
Rais Mohamed Morsi ambaye alipigiwa kura na Wamisri kupitia chama cha Muslim
Brotherhood amesalia gerezani mpaka kesho.
Nchi za Magharibi
zikiongozwa na baba yao mkubwa Marekani zimekaa kimya mpaka apo jana Rais
Barack Obama aliposema kwamba Marekani inasitisha mazoezi ya kijeshi na Misri.
Wamisri wameedelea kuuwawa, kuteseka, kusalia majiani, uchumi wa Misri
umeendelea kuporomoka na mahusiano kati ya watu wa dini mbali mbali nchini
Misri yameendelea kuwa mabaya zaidi.
Tukirudi kwenye
historia tukaangaza kinachotokea Misri wengi tunaweza kusema ni mpango mzima
ulioandaliwa kwa muda mrefu na nchi za Magharibi lakini Wamisri wao hawakuweza
kuangaza macho mapema. Lugha nzuri ya Kimagharibi yenye kuongelea Demokrasia
ikiwa imefungwa na maboksi mazuri ya misaada iliwapumbaza Wamisri.
Nasema hivyo kwa mfano
mdogo sana wa Watawala wa Misri kwa sasa. Katika uchaguzi ulioitwa wa
kidemokrasia wagombea maarufu wawili ni wasomi waliosomea hapa Marekani.
Mohamed Morsi amesoma University of Southern Calfornia, na Mohamed El Baradei
alisomea New York University. Wote wanaelewa ni kitu gani unapoongelea demokrasia
kadiri ya Wamarekani au nchi za magharibi.
Mohamed Morsi kwa
kujiunga na Muslim Brotherhood kwa macho na mtizamo wa Wamarekani alikuwa
amejichafua, na mara moja Wamarekani na nchi za Magharibi wakayaelekeza macho
yao kwa Mohamed El Baradei na kuweka matumaini kwamba atashinda. Lakini
mategemea yao yaligonga mwamba, baada ya Mohamed Morsi kukamata dola la Misri.
Choko choko ilianzia hapo.
Wakaja na sababu ambayo
si ya kweli na kusema kwamba kwa kuwa Muslim Brotherhood wameshinda Madheebu ya
Kikristo yatakuwa kwenye shida ya kuwindwa na Waislam. Waliendelea kulazimisha
sababu hiyo na kuiaminisha dunia nzima kwamba ni kweli. Jambo ambalo alikuwa na
mashiko. Kwani Waislamu na Wakristo ndani ya Misri wameishi pamoja toka enzi
kabla hata hivyo vijisenti vya Marekani avijaanza kupelekwa Misri
Kupinduliwa kwa Mohamed
Morsi ilikuwa ni matokeo ya visingizio
vya Kimagharibi ambavyo daima utupeleka pabaya. Tamaa za Waafrika hasa wachache
kwa kukubali vijisenti na kuuza haki za walio wengi ndio matokeo tuyaonayo
Misri leo.
TANZANIA JE? Ndugu
zangu watanzania tuna mengi ya kujifunza kutoka Misri tena kwa umakini zaidi.
Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alisema “Ubepari ni Unyama” mpaka
kesho kuna watu wanaendelea kumlaumu kwa kauli hii. Lakini ningewaomba wale
ambao wanamlaumu wachukue muda kufikiria hali ya Misri na Zimbabwe.
Hivi karibuni
Watanzania tulipata bahati ya kutembelewa na Marais watatu wa Marekani tukianza
na Rais Barack Obama, na marais wastaafu George Bush na Bill Clinton. Kwetu
ilikuwa furaha kwani Marekani ni nchi kubwa na ni muhimu sana kwetu kuwa na
mahusiano mazuri na Marekani.
Lakini swali moja
ambalo tunajiuliza kimya kimya bila kupaza sauti, NI KWANINI WAMECHAGUA TANZANIA? Hapo
tutatofautiana sana kwa majibu kwani wengine twaeza kuwa na mitizamo tofauti
katika suala hili. Kuna wanaosema kwa kuwa Tanzania ni kisima cha amani,
wengine wanasema Tanzania tumekuwa mstari wa mbele katika utetezi wa haki za
binadamu. Majibu yote yanavutia na ni ya kweli kwa kiasi fulani
Sisi tuliopata bahati
ya kuishi nchii hii (Marekani) twaweza kuwa na majibu mazuri zaidi kuliko labda
wale wanaoishi nyumbani. Ndugu zangu hapa Marekani kuna omba omba, watu
wasiokuwa na makazi (homeless), ulala majiani, shule zinafungwa kwa sababu ya
kukosa pesa, watu wanajipanga kwenye msululu wa kutibiwa kwa sababu hawana bima
ya maisha, watu wanajipanga kupata chakula cha msaada (food pantry) na mengi mengineyo.
Lakini cha kushangaza
nyumbani tunapewa Mamilioni ya pesa ya msaada. Na bila kujiuliza tunapiga
makofi na kuwachezea ngoma. Hayo hayo mamilioni ndio yanayoimaliza Misri kwa
kivuli cha demokrasia. Najua sisi tulio wengi upenda furaha ya muda mfupi na
saa nyingine ni vigumu kwetu kuangaza mbali na kuzifanya hakili zetu zifikirie
mbali zaidi zaidi ya leo.
Ndugu zangu Wamisri
waliishi pamoja hata kabla ya Taifa la Marekani kuzaliwa, leo hii wanaambiwa Waislam wanawachukia
Wakristo, na wao kwa sababu wameishakubali mapesa yao inabidi wakubali. Kwahiyo
na Wamisri wamekubali kwamba ndio kuna chuki kati yao. Na bunge la Marekani
linaongelea kuwapa ifadhi Wakristo wanaoteseka huko Misri. Jamani chuki hiyo
imezaliwa siku mbili hizi?
Tanzania je?
Tunayoyaona Misri Tanzania yameanza, chokochoko ndogo ndogo za kisingizio cha
dini. Tunasikia nchi inaongozwa na mfumo Kikristo, achinje nani? Polisi
wanaonea dini fulani. Taratibu mambo haya tunayaona na kuyasoma kwenye vyombo
vyetu vya habari. Siwezi kusema yameletwa na Marekani lakini kama Mwl. Nyerere
alisema ukweli kwamba ‘Ubepari ni Unyama’ na kama mabepari wameishavamia nchi
yetu basi hapo kuna kitu. Inawezekana wameishasambaza unyama wao.
Watupumbaze kama
walivyowapumbaza Waafrika Kusini kwa kuwapa Uhuru hewa na mpaka leo Waafrika
kusini asili ni masikini wa kutupwa ingawa uchumi wan chi huko juu. Na Sisi
watupumbaze wakituacha tukigomabana kuhusu Nani Achinje, Nani Bora kati ya
Mkristo na Mwislam, wakati huo huo maliasili yetu ikiamia katika nchi zao za
Magharibi.
Watanzania wenzangu
lazima kufungua macho yote mawili bila kufumba, lazima kuamuka na kujivunza
kutoka kwa wenzetu sio kila kingaacho ni zahabu. Lengo letu ni kuhakikisha kila
mtoto wa Mtanzania anakwenda shule, anatibiwa na anapata lishe. Kwamba ni
Mwislam au Mkristo alijawahi kuwa tatizo letu, kwa nini liwe leo. Kuna
kajiswali muhimu hapo.
Ndugu zangu wakati
wenzetu Wachina na Wahindi wanasambaza Mainjinia duniani kote Sisi kazi yetu ni
kusambaza wataalamu wa kuuza Madawa ya Kulevya!!!!! Lazima tujiulize na kuanza
kujipanga, tamaa ya wachache itatutumbukiza kwenye haya tuyaonayo Misri.
Ndugu zangu Waislamu na
Wakristo kwa pamoja lazima kupaza sauti na kusema kwa pamoja kwamba hili
hapana, la sivyo Umisri unatunyemelea.
Yangu ni hayo-Karibu
kwa maoni.
3 comments:
umemaliza yote ndugu mwandishi ni kweli yote ulioyaandika lakini watanzania wenzangu watakuelewa?Mungu ibariki Africa Mungu bariki TANZANIA NA VIONGOZI WAKE UWAPE UFAHAMU YA KUONGOZA WATU NA SERA NZURI
OMG Jesus Christ. I`m crying for your message, because everything is true. And I`m saying as a Christian person and I do live in USA.
My Brother/ Sister Sometimes I just wish people they could see the truth and I do pray for that. Tanzania is a very good country and I love it with all my heart, I`m so proud to be Tanzanian because I feel like I`m unique different unlike other country. Its true the way country it is now not so good like it used to be . I blame to the all Tanzanian leaders who are very selfish,ungrateful who don`t care their people and middle class at all. They promised and don't keep their promises.
They do have everything they wanted but stills refuse to hear Middle class voice. Sometimes I wish God to eliminate all leaders who don't do fair to their own people. Now these days if you are middle class , poor need help you cant get help. But if you have a popular name and need help you will see all leaders will help because you are rich like them, hello what about us. I'm just praying to God through Jesus Christ to hear Middle Class`s tears, Lord we need your Hand oh Jesus come and wipe our tears away . We are so tired oh Lord with Evil doing from selfish Leaders. Jesus please come to take your Holly Church in Jesus Name Amen.
Tanzania inabidi tuchange true demokrasia ya ukweli siyo mambo ya kurithi njenje au a few always in power abd never retire. Rushwa za kijinga hazitufikisha popote zaidi ya umaskini kiakili...time tanzania iwe for tanzanians siyo watu weingine using tz passports na kubba madawa au upuuzi mwingine...and pay the real teachers, police and mostly the doctors
Post a Comment