ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 11, 2013

YANGA MOTO CHINI SC VILLA YALAZWA 4 -1

Timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, leo imemaliza vyema mechi zake za Kimataifa za Kirafiki za kujipima nguvu, baada ya kuigalagaza timu ya Sports Club Villa ya Uganda kwa jumla ya mabao 4-1 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 


Katika mchezo huo, hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa wakiongoza mabao 3-1, yaliyofungwa na Mrisho Ngassa, katika dakika ya saba kwa shuti kali alilopiga akiwa nje ya kumi na nane, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 27 kwa mpira wa adhabu ndogo alioanziwa na Niyonzima na Jerry Tegete katika dakika ya 30, aliyemtoka beki wa Villa na kupiga mpira uliogonga mwamba wa juu na kudunda nyuma ya mstari na kumaliziwa na Didier Kavumbangu. 


Bao la nne lilifungwa na Haruna Niyonzima katika dakika ya 62, baada ya pasi nzuri aliyocheana na David Luhende aliyetiririka winga ya kushoto akimtoka beki wa Villa na kumimina crosi matata iliyomkuta tena Niyonzima, aliyetulia vilivyo na kumchambua kipa wa Villa, aliyekuwa akijaribu kutoka golini ili kupunguza ukubwa wa goli.


Bao la kufutia machozi la Sports Villa, lilifungwa na Moses Ndaula katika dakika ya 18. 
Katika mechi zake za awali za kujiandaa na msimu, Yanga SC ilitoa sare ya 2-2 na URA ya Uganda kabla ya kuzifunga 3-1 Mtibwa Sugar na 1-0 ikiifunga 3Pillars ya Nigeria. 


Kufuatia ushindi huo, Yanga imejiweka katika nafasi nzuri ya kuwakabili wapinzani wao Azam Fc katika mchezo wao wa Jumamosi ijayo wa kuwania Ngao ya Hisani.

No comments: