ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 11, 2013

SHEIKH PONDA AKIWA HOSPITALI YA MUHIMBILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MOROGORO LATOA TAMKO

Sehemu ya kodonda katika bega la Sheikh Ponda baada ya kushinwa nyuzi.
Katibu wa Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, akiwa katika Wodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akitibia jeraha alilopata jana akidaiwa kupigwa risasi mjini Morogoro.
Sheikh Ponda akiwa hospitalini hapo na jeraha katika bega la mkono wa kulia.
Sheikh Ponda akiwa na msaidizi wake hospitalini hapo.
TAMKO LA JESHI LA POLISI KUHUSU SHEIKH PONDA ISSA PONDA


1. MNAMO TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA KONGAMANO LA BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.


2. KONGAMANO HILO LILIFUNGWA MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA ENEO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI.


3. BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA KUWARUSHIA MAWE ASKARI. KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO, ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.


4. KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA. HIVI SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.


5. KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI CP ISSAYA MNGULU IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.


6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.


Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.

4 comments:

Anonymous said...

Pumbavu..... "suala linashughulikiwa kisheria" nani anaejuwa sheria? Serikali gani ilio na sheria Tanzania? Jeshi la polisi sheria wanayo wao mkononi. Leseni walizonazo sio za kutumia silaha bali ni leseni za kuuwa. Kikwete we ni muislamu jina tu. Unakaa ukiacha waislamu wateswe na wasiwe na haki ya kuongea au kuitetea dini watakavo. Lakini mutambue kuwa dunia ni mapito tu, hapa duniani nyie mmeshika mpini ila akhera mtashika makali.

Anonymous said...

Tanzania sio nchi ya kiislamu na hatukumchagua kikwete awe shehe... wewe anonymous ndo mpumbavu kweli, acha sheria zifatwe. wewe kama mujaheedena kajifunge mabomu ufe kwa ajili ya mungu asiye weza kujitetea... halafu ziwa la moto hilo hakuna vimwali huko.

Anonymous said...

Wewe Anonymous wa kwanza kabisaaaa katika hii mada unamatatizo ya Akili wahitaji kuripoti Mirembe Hospital harakaaa sana ! rais Kikwete hakupigiwa Kura na waisilamu tu bali alipigiwa na wa Tanzania woote na si kupigania haki za Waisilamu pekee Bali Taifa zimaaaa la Tanzania! haijalishi dini wala rangi ni lazima kuheshimu utu wa mtu hata kama humpendi! Haijalishi wewe Muisilamu au mkristo heshima ni Muhimu sana na UGaIDI ni dhambi kabisaaaa tena Serikali haitovumilia hata kidogo!!! Na Kutangaza chuki si haki ni kinyume cha Utanzania hivyo watapigwaaaaaaaaaaa woooote wasio tiii Amri na Sheria za chi yetis ya Tanzania! Msituleteeee uvurugaji wa Amani hapa. Hatutakubaliiii kabisaaaaaa!!!!

Anonymous said...

Hiviiii ni kwanini Hawa mashehe wana leta vurugu nchini kweetu???? Kwani Tanzania si ni ya Watanzania woooote jamani? Inakuwaje wao wana jifanya Kuwa Tanzania ni ya Waislamu tu? Na ni kwanini fujooo nyingi wanazifanya Waisilamu? Inamaaana Dini ya Kislamu na Quran vinaruhusu kumwaga damu jamani na inaruhusu uvurugaji wa Amani??? jamani mnafunga na kusali ili kuvuruga Amani,Upendo na umoja??? sHAME ON YOU! Na Mungu atawalaaani tu nyie woooote wavuraga Amani!!!!!