Baada ya kuachiwa kwa dhamana na kurudi uraiani video queen,Agness Masogange na Melisa Edward waliokamatwa kwa kutuhumiwa kubeba dawa za kulevya huko Johannesburg, Afrika Kusini,Masogange amepost picha mtandaoni kwa mara ya kwanza ili kuwathibitishia mashabiki wake kuwa ni kweli yupo huru.
Picha hizo zinamuonyesha Masogange akiwa gym akifanya mazoezi.
Hata hivyo habari kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Dawa za Kulevya Afrika Kusini, Kamishna Toto Mangaleni aliithibitisha jana kuwa watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana,lakini wataendelea kubaki Afrika Kusini wakati kesi yao ikiendelea.
Mangaleni alisema wanawake hao ambao juzi pia walipanda kizimbani, walipata dhamana hiyo jana kutoka Mahakama Kuu ya Gauteng iliyoko eneo la Kempton Park jijini Johannesburg.
Hata hivyo, Kamishna Mangaleni alisema hawezi kuzungumzia zaidi kuhusu kesi hiyo kwa sababu hataki kuharibu uchunguzi ambao unaendelea dhidi ya Watanzania hao, ambao ni wasanii.
Marafiki wa karibu wa Masogange wanaoishi maeneo ya Midland Johannesburg ambao walikataa kunukuliwa majina yao, walithibitisha kuwa wanawake hao wameachiwa kwa dhamana.
“Ni kweli wameachiwa leo asubuhi. Lakini hatuwezi kuongelea kwa kina habari hizi kwa sababu hatutaki matatizo na polisi. Hii kesi bado inaendelea na wataendelea kubaki hapa hadi kesi yao itakapomalizika,” alisema mmoja wa marafiki zake.
2 comments:
Kuwa huru si hoja dada bado wewe ni mharibifu na wala sio ushujaa. you did it.
Binti umekuwa huru unatutangazia ili tukueleweje? huna ufahari zaidi ya kuonekana muuza unga. Hatuhitaji kujianika kwako kuwa mtulivu ujue hatima yako ninini! Au hao walokutuma wanafanya kazi ya kukuhongeshea???
Post a Comment