Ni habari njema zilizoeneza zaidi ya wiki tatu zilizopita kuhusu show mpya ya TV ambayo inaongozwa na mwigizaji Mtanzania Irene Uwoya.
Irene kupitia AMPLIFAYA ya Clouds FM alitangaza kuacha kuigiza movie na sasa atawekeza muda wake kwenye show ya TV ambayo imelenga kukarabati nyumba mbovu za Watanzania.
Utaratibu anaoutumia ni kupokea maombi ya Watanzania wanaohitaji nyumba zao kukarabatiwa alafu Irene na timu yake ndio wanachagua nyumba ya kuikarabati, huduma ambayo wanaitoa bure….
Hii video hapa chini ni sehemu ya mfululizo wa show ya Irene Uwoya ambayo inaonekana @Clouds_TV peke yake.


1 comment:
Kazi nzuri sana.Kipindi kipya bongo safi sana mbarikiwe.Ila mtizamo wangu mimi naona kuna watu ambao kwa kweli wanaishi kwenye nyumba mbovu sana kulinganisha na hiyo.Jamani tips tuu Naomba muende bagamoyo Mtoni kijiji cha wakimbizi hapo naona watu wanahitaji sana msaada.Jamani kuna watu wanaishi kwenye nyumba ambazo mazingira ni hatari kwa jamii.
Post a Comment