ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 20, 2013

PETE YA NDOA IMENIPONZA....NDOA IPO HATARINI

Wadau nipo njia panda naombeni ushauri wenu, nimefanya kosa kubwa na nalijutia
Tafadhali naomba ushauri badala ya kunituhumu
Mwezi nilikuta na demu mmoja tulisoma naye chuo kitambo alikuwa demu wangu for time being, so baada ya miaka kadhaa tukaja kukuta sehemu, shetani akanipitia nikavunja amri ya sita naye
Baada ya kurudi home nikagundua sina pete, nikajaribu kukumbuka nilipoiweka sikupata majibu
Baada ya siku kadhaa yule demu akzidi kunisumbua na kutaka niwe karibu naye sana lakini nikaona si vyema maana anaweza kusababisha mtafaruku kwa ndoa yangu
Baada ya kuona nampotezea akaniambia sasa unajifanya mjanja pete yako ni nayo na nahitaji sh 500,000 cash ama sivyo naharibu kwa mkeo kwamba pete ninayo na ulinikopa.
Kibaya zaidi wife aliniuliza pete umepeleka wapi nikadanganya nimeisahau ofisini nilikuwa nafungua printer sasa pete ikawa inani disturb nikaivua , nilipoenda jumatatu nikamwambia nahisi wahudumu wa usafi wameiiba maana siiona pale nimeiweka naendelea na uchunguzi.

Mwanzo nilimpuuzia lakini mshenzi yule kapeleleza hadi wife anapofanya kazi na kapata simu yake, juzi kampigia kamwambia "naomba mkumbushie mumeo deni langu mimi xxxxx nampigia simpati" halafu akakata simu.
Niliporudi wife kanibana nikamwambia ni mambo ya kazi tu akataka kujua no yake kaipataje, nikazuga zuga na ubabe wa kiume yakaisha

Nikipiga akili nimuendee Polisi naona kama kitanuka na wife atajua
Nikifikiria kumlipa akili hainipi kabisa....kilo tano?
Sijui nimueleze wife ukweli?

Nimejaribu kumpiia simu na kumbembeleza kagoma anachohitaji ni kilo tano au aniharibie kwa wife
Tafadhali ushauri wakuu lawama na madongo hayatanisaidia

3 comments:

Anonymous said...

Mie naona umweleze wife na umuombe msamaha. Waeza mpa pesa huyo demu na bado akamwambia mkeo vilevile. Ila na wewe ndo utosheke na mkeo!

Anonymous said...

Kwanza wewe ni msaliti na inabidi uache mara moja tabia hio hasa ukizingatia una mke wa ndoa. Pili wanawake wako wa namna nyingi na kila mmoja na alivoumbwa sasa mie nitatoa ushauri kama mie na sijui mkeo yeye yukoje. Kama ni mie basi mume anieleze ukweli yeye mwenyewe naweza nikamsamehe kulikoni nikaja kusikia kwa wengine. All the best

Anonymous said...

USHAURI WANGU NIHIVI MWAMBIE WIFE UKWELI JUU YA HILO TATIZO NA USIFICHE, KAMA NIMTU MUELEWA ATAUMIA KIDOGO THEN ATAPOTEZEA. ILA UACHE TABIA ZA AJABU NA WEWE