ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 20, 2013

UFUNGUZI WA TAWI LA CCM - CALIFORNIA MHE. MWINGULU NCHEMBA AWASIFIA WAKEREKETWA

Mhe. Mwigulu Nchemba akiwaeleza machache wakereketwa wa CCM katika jimbo la California. Meh. Nchemba alifanikisha zoezi la ufunguzi tawi la CCM - California
Mwenyekiti wa tawi la CCM - California  Josephine M. (kushoto) akiwa ana teta na Katibu wake Erick B. wakati wa sherehe wa ungunguzi wa tawi la CCM - Californa.

Mwenyekiti wa CCM tawi la California - Jospehine M (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mhe. Mwigulu Nchemba kabla ya kumtambulisha rasmi kwa wanachama,
























































6 comments:

Anonymous said...

Kwa Tanzania kupiga kufanya mageuzi ya kidemokrasia, kiuchumi na kijamii ni lazima CCM ife.. Ikae pembeni ...mifano ni mingi tu.. Tuangalie majirani zetu kwanza!! Inasikitisha hata baada ya kupata fursa ya kuishi nchi iliyoendelea na ya kidemokrasia bado tunakumbatia CCM: ( Ubinafsi umetujaa... Hatufanani hata chembe na wenzetu nyumbani wanaoteseka kwa utawala wa CCM!

Anonymous said...

Mdau unaposema mifano ni mingi na bila kutoa hata mfano mmoja hai, unaondoa maana nzima ya ulichokiandika. Sasa toa hiyo mifano na andika hizo nchi ya majirani. Ni vuzuri kushuka nyanga nzima ili wadau tukusome vizuri. Lah asha utakuwa ni ushabiki mtupu hapa.

Anonymous said...

Kama unataka nikufundishe na mifano uelewa wako ni mfupi sana... Mimi si shabiki wa chama niko US na maisha mazuri tu... Pitia historia ya siasa za Africa utapata jibu! Kwa kukudokezea tu vyama vikongwe havina tija... Vinatabia ya kujisahau :( wenzetu Kenya waliiweka pembeni KANU!!! Waangalie walipo wameweza kujenga katiba yenye manufaa kwa wananchi wote was Kenya!! Tanzania ni nchi yangu ninaipenda na kuitakia mema... Unahitaji kipi ili uchukie utawala wa CCM? Kama huna macho pole... Kila aitakiae mema Tanzania hawezi kufurahishwa na CCM ya Leo...nafikiri upeo wako mfupi ndiyo unaokupa ushabiki!!!

Anonymous said...

mimi ni Mtanzania na nipo hapa Oakland California ilipokuwa raisi wetu, ni kweli kabisa CCM washindwe ili waamke, mimi niliwauliza hawa jamaa ni nini manufaa ya hili tawi la CCM kwa watanzania hapa california na kule nyumbani ? hakuna alinipa jibu sahihi. nikajua hii ni vitongoji vya kutumia pesa za walipa kodi wa huko nyumbani. wizi mtupu na ufujaji wa Tanzania tax payer.

Anonymous said...

Mdau sasa kama unaishi marekani maisha mazuri nadhani inakuwa mtu mbinafsi kama unajipenda mwenyewe bila kuaangalia Hali za ndugu zako. Nadhani suala la kumchungulia jirani yako anafanya nini na wewe uweze kuiga, nikupe pole msuada huo umepitwa na wakati.

Anonymous said...

Nadhani mkaaji wa Oakland ulishindwa au umepitiwa kidogo. Soma Katika CCM madhumuni ya matawi CCM. Punguza maneno ya mtaani. Tumechoshwa na story za mtaani na tunahitaji chombo CCM ambacho kitatupelekea mapemdekezo yetu kwa wahusikika. Story za domokaya mtaani hazina deal. Mjini shule mdau njoo nikupige shule. Sasa tunaelekea Chicago!