JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu ya mdomo: 255 22 2460
735/2460 706-8
FAKSI: 255 22 2460 735/700 S.L.P.
3056
Unapojibu
tafadhali nakili:
Ref. No.:
TMA/1622 6
Septemba, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA OKTOBA - DISEMBA 2013 NCHINI
Taarifa hii inatoa tathmini ya mvua za masika (Machi
- Mei) 2013 na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa na mvua kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2013.
1.0 TATHMINI
YA MVUA KIPINDI CHA MACHI – MEI, 2013
Katika msimu uliopita wa mvua za masika 2013, maeneo
mengi ya nchi yalipata mvua za wastani
isipokuwa maeneo machache ya mikoa ya Tabora, Rukwa, Mara na Singida ambayo ilipata mvua juu ya wastani. Wakati huo
huo baadhi ya maeneo ya mikoa ya Iringa, Ruvuma, Kilimanjaro na maeneo mengi ya
mwambao wa pwani yalipata mvua chini ya
wastani.
Vifuatavyo ni viwango vya mvua pamoja na asilimia ya mvua
zilizonyesha ikilinganishwa na wastani wa muda mrefu katika baadhi ya vituo nchini:
1.1 Maeneo yanayopata misimu
miwili ya mvua kwa mwaka
Kanda ya Ziwa Victoria: Bukoba milimeta 984.9 (110.9%),
Mwanza 385.0mm (101.1%), Musoma milimeta 516.4 (127.5%), Ukiriguru milimeta 363.4
(107.5%) na Shinyanga milimeta 307.7 (61.1.0%).
Nyanda za juu kaskazini
mashariki: Arusha milimeta 368.8 (84.4%), Moshi milimeta 472.9 (77.9%), Lyamungo milimeta
655.5 (65.3%), Kilimanjaro milimeta 291.6 (95.5%) na Same milimeta 291.3 (111.8%).
Pwani ya kaskazini na
visiwa vya Unguja na Pemba: Zanzibar milimeta 534.3 (62.0%), Amani milimeta 484.0
(63.0%), Kizimbani milimeta 667.7 (75.2%), Dar es Salaam milimeta 458.8 (77.7%),
Morogoro milimeta 227.8 (55.1%), Tanga milimeta 586.7 (91.4%) na Pemba milimeta
884.0 (85.7%).
1.2 Maeneo yanayopata msimu
mmoja wa mvua kwa mwaka:
Nyanda za juu kusini magharibi: Mbeya milimeta 254.8 (85.7%),
Sumbawanga milimeta 275.0 (126.2%),
Mahenge milimeta 1215.5 (118.2%) na Tukuyu milimeta 1094.2 (96.7%).
Kanda
ya magharibi: Tabora milimeta 296.4 (135.2%), Kibondo milimeta 418.2 (94.0%) na Kigoma milimeta 318.7 (94.6%).
Pwani
ya kusini: Kilwa milimeta 346.4 (68.3%), Mtwara milimeta 404.2 (86.0%) na Naliendele milimeta 350.5 (79.4%).
Kanda
ya kati: Singida milimeta 410.0 (198.9%), Dodoma milimeta 145.1 (82.0%) na Hombolo milimeta 101.0 (52.9%).
Kanda ya kusini:
Songea milimeta 247.9 (67.5%)
Viwango vya mvua chini ya asilimia 75 ya wastani kwa
kipindi kirefu hutafsiriwa kama chini ya wastani, wakati viwango vya kati ya
asilimia 75 na 125 hutafsiriwa kama mvua za wastani na vile vya zaidi ya
asilimia 125 hutafsiriwa kama juu ya wastani.
2.0 MWELEKEO WA MVUA KIPINDI CHA OKTOBA – DISEMBA 2013
2.1 Utangulizi
Wanasayansi kutoka taasisi za hali ya
hewa kwenye nchi za Pembe ya Afrika, Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, na
taasisi za kikanda na kimataifa walikutana Nairobi na baaadae Eldoret, Kenya kuanzia
tarehe 12 hadi 23 Agosti, 2013 kufanya uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa na
kutoa mwelekeo wa mvua za msimu katika ukanda huu. Aidha, mkutano kama huo
ulifanyika pia kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) huko
Harare, Zimbabwe kuanzia tarehe 19 hadi 31 Agosti, 2013 ambapo Tanzania ilishiriki. Mikutano hiyo ilikuwa inafanyika
sambamba na mkutano wa wataalam na wachambuzi wa masuala ya hali ya hewa na
klimatolojia katika Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambapo tathmini ya kina katika mifumo ya hali ya
hewa na athari zake kwa msimu ujao wa
mvua nchini ilifanyika.Viashiria vikuu vilivyotumika ni pamoja na hali ya joto la Bahari katika maeneo ya bahari
ya Hindi, Atlantiki pamoja na yale ya tropikali ya bahari ya Pasifiki.
2.2 Mifumo ya hali ya hewa
Joto
la Bahari lililopo na linalotarajiwa katika maeneo ya tropikali ya bahari za
Pasifiki, Atlantiki pamoja na Hindi lilichambuliwa. Viashiria vingine ikiwemo mifumo
na mwelekeo wa upepo ambayo huleta unyevunyevu katika nchi yetu pia ilizingatiwa.
Katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2013 joto la wastani hadi chini ya
wastani linatarajiwa katika maeneo ya tropikali ya bahari ya Pasifiki.
Hali
ya joto la bahari inatarajiwa kuwa juu kidogo ya wastani katika maeneo ya
mashariki mwa Bahari ya Hindi (pwani ya Indonesia) katika miezi ya Oktoba hadi
Novemba 2013, ikiambatana na hali ya joto la bahari chini kidogo ya wastani
katika maeneo ya magharibi mwa Bahari ya
Hindi (pwani ya Afrika Mashariki). Hali
hiyo inatarajiwa kusababisha upepo wenye
unyevunyevu hafifu kutoka bahari ya Hindi kuelekea katika maeneo mengi
ya pwani ya Afrika mashariki. Aidha, upepo kutoka magharibi katika misitu ya
Kongo unatarajiwa kuwa hafifu na hivyo kupunguza kiwango cha unyevunyevu angani
katika maeneo ya magharibi mwa nchi.
Hata hivyo, katika kipindi cha mwishoni mwa miezi Novemba hadi Desemba, 2013
kunatarajiwa kuwa na ongezeko la joto la bahari katika eneo la magharibi mwa Bahari ya Hindi hali hii
inatarajiwa kusababisha ongezeka kiasi la unyevunyevu katika maeneo ya ukanda
wa Pwani ya Afrika Mashariki.
Ongezeko kiasi la joto la bahari kusini-magharibi mwa
bahari ya Hindi katika kipindi cha Novemba na Disemba, 2013 linatarajiwa
kusababisha kuwepo kwa matukio ya vimbunga katika kipindi cha msimu wa mvua za vuli, na hivyo kuathiri mifumo ya hali
ya hewa nchini katika vipindi vifupi.
2.3 Mwelekeo wa Mvua Oktoba
- Disemba 2013 Kutokana na mwelekeo wa mifumo ya hali
ya hewa kama ilivyoelezewa hapo juu, mvua za kipindi cha Oktoba hadi Disemba,
2013 zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:
(i)
Mvua za Vuli (kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua)
Msimu
wa mvua wa Oktoba hadi Disemba (Vuli) ni mahususi katika maeneo ya nyanda za
juu kaskazini mashariki, pwani ya kaskazini, kanda ya Ziwa Victoria na
kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
Mwaka
huu mvua zinatarajiwa kuwa chini ya wastani katika maeneo ya pwani ya kaskazini
(mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, pamoja na
visiwa vya Unguja na Pemba), nyanda za juu kaskazini mashariki (mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha na Manyara), mikoa ya Mwanza, Simiyu na Shinyanga,
maeneo ya kanda ya Ziwa Victoria (mikoa ya Kagera, Geita na Mara),
kaskazini mwa mkoa wa Kigoma pamoja na baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa mikoa ya
Arusha na Kilimanjaro yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani.
Kanda ya Ziwa Victoria: (Mikoa ya
Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga): Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili ya mwezi
Septemba, 2013 katika mkoa wa Kagera na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma na
kuendelea kusambaa katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita na Simiyu
katika wiki ya tatu ya mwezi Oktoba, 2013. Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani
katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mara na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Katika
mikoa mingine ya ukanda wa Ziwa Victoria (Mwanza, Shinyanga, na Simiyu) mvua
zinatarajiwa kuwa chini ya wastani.
Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (Mikoa ya
Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na
Pemba): Mvua zinatarajiwa kuanza wiki
ya tatu ya mwezi wa Oktoba, 2013. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za chini wastani
katika maeneo mengi.
Nyanda za juu Kaskazini Mashariki:
(Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara): Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Oktoba,
2013 na zinatarajiwa kuwa chini ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya
Kilimanjaro, Manyara na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Arusha. Hata hivyo
kaskazini mwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, mvua zinatarajiwa kuwa za wastani
katika baadhi ya maeneo.
(ii) Mvua
za Msimu (Novemba – Aprili) kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua.
Msimu
wa mvua za Novemba hadi Aprili ni mahususi katika maeneo ya magharibi mwa nchi,
kati, nyanda za juu kusini-magharibi, kusini mwa nchi na pwani ya kusini.
Katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2013 maeneo mengi yanatarajiwa kupata
mvua za wastani.
Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma,
Tabora, Katavi na Rukwa):
Mvua
zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Oktoba, 2013 katika mkoa wa Kigoma na
wiki ya tatu ya mwezi Novemba, 2013 katika mikoa ya Tabora, Rukwa na Katavi.
Mvua hizi zinatarajiwa kuwa za wastani katika maeneo ya kusini mwa mkoa wa
Tabora na maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Rukwa. Mikoa ya Katavi, kusini mwa
mkoa wa Kigoma, magharibi mwa mkoa wa Rukwa na kaskazini mwa mkoa wa Tabora, mvua zinatarajiwa kuwa chini ya wastani.
Kanda ya kati (Mikoa ya Singida na
Dodoma):
Mvua
zinatarajiwa kuanza wiki ya pili ya mwezi Disemba, 2013 na zinatarajiwa kuwa za
wastani katika maeneo ya kusini na uwezekano mkubwa wa kuwa na mvua chini ya wastani
katika maeneo ya kaskazini mwa mikoa hiyo.
Nyanda za juu Kusini Magharibi: (Mikoa
ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro):
Mvua
zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Novemba, 2013 na zinatarajiwa kuwa za
wastani katika maeneo mengi.
Maeneo ya kusini na pwani ya kusini
(mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara)
Mvua
zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Novemba, 2013 na zinatarajiwa kuwa za
wastani na upo uwezekano wa baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Lindi
kuwa na mvua chini ya wastani.
No comments:
Post a Comment