Mtu anaonekana amevunjika mguu hapa akibebwa nawasamalia wema tumaini ni kuwa ajasachiwa maana bongo ajari ikitokea baada ya kupata msaada unajikuta umepoteza kila kitu chako.
Ajali mbaya nyingine imetokea usiku huu katika mlima kwa Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa katika barabara kuu ya Dar es Salaam -Iringa .
Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo huku wa wawili wakijeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana uso kwa uso .
Ajali hiyo imetokea mida ya saa 12.50 jioni ya leo ikiwa ni dakika takribani 30 baada ya ajali ya basi la JM kupinduka eneo la Mazome wilaya ya Kilolo.
waliopoteza maisha katika ajali hiyo ambayo chanzo ni dereva wa lori la IT lililokuwa likisafirishwa kwenda nchi za kusini mwa Tanzania aliyekuwa akitaka kulipita gari la mbele mlimani na katika kona kali .
Hata hivyo dereva wa lori hilo IT aliyetambuliwa kwa jina la Gody amevunjika mguu wake ambao umetoka katika na dereva na utingo la fuso wamekupa papo hapo huku mwanamke aliyekuwa katika lori IT akisalimika .
habari zaidi itakujia
1 comment:
Tunashukuru sana tena sana Bwana Lucas kwa kanzi nzuri unayoifanya katika jamii yetu. Kazi ambayo haistahiki kuvunjwa kuvu kabisa. Isitoshe naomba uchukue ushauri huu kwa ni asafi na kwa lengo la kukiimarisha chombo hiki. Ningeshauri picha kama hizi zivunikwe hizo sehemu za majeraha. kuwe na kiwango cha uoneshaji matukio kama haya, kwani yanatisha sana, na kuogopesha.
Ahsante
Post a Comment