Advertisements

Wednesday, October 16, 2013

AUNTY LULU AKOBWA VITU DUKANI, AKIMBILIA BAGAMOYO NA ATOA ONYO KALI..

MSANII wa filamu za Kibongo ‘Aunty Lulu’
 Lulu Semagongo aliyeibukia kwenye utangazaji, amekombwa vitu kibao vya thamani dukani kwake na watu wasiojulikana.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilitokea wiki iliyopita, usiku wa manane katika duka la msanii huyo lililopo Kinondoni – Biafra jijini Dar es Salaam ambapo vitu vilivyoibwa ni pamoja na viatu, nguo, pochi, simu na fedha.
“Kwa kweli nimechanganyikiwa sana, hadi sasa bado sijajua thamani ya vitu vyote kwa jumla ni kiasi gani lakini nasema sitaki lawama. Walioniibia ni heri wanirudishie tu kwa njia yoyote maana kitakachowakuta hawatasahau.
“Nimeshakwenda Bagamoyo kwa mtaalamu wangu na kazi imeshakwisha. Natoa siku saba vitu vyangu viwe vimerudi vinginevyo...” alisema Aunty Lulu bila kufafanua zaidi.
GPL

No comments: