“Nilikuwa nimelala ndani, nilipoamka asubuhi nilikuta mlango umefungwa kwa nje hata hivyo nilivumilia hadi njaa ilipoanza kuniuma baada ya siku tano nikaanza kupiga kelele ndipo majirani walipokuja kunifungulia na kuniambia nyumba imeuzwa” alisema mtoto Erasto Emmanuel pichani juu.
Mtoto Groly Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Hatwelo alisema aliagwa na baba yake ambaye alimwachia shilingi 3,000 lakini hakumwambia kama nyumba imeuzwa.
Barua ya makubaliano ya kuuziana kiwanja chenye nyumba ndani yake.
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Yasin Yuta, alisema majirani waligundua baada ya kusikia kelele za mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Erasto Emmanuel (11) aliyekuwa amefungiwa ndani na kukaa kwa siku tano.
VITENDO vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea kushika kasi katika baadhi ya maeneo hususani vijijini, licha ya Serikali na asasi mbalimbali kulipigia kelele ambapo hivi karibuni Baba mmoja aliamua kuuza nyumba ikiwa na watoto ndani na kutokomea kusikojulikana na kuwaacha wasijue la kufanya.
Mkasa huo wa ajabu ulitokea katika kijiji cha Hatwelo, Kata ya Ijombe Mbeya Vijijini ambapo Mkazi huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Yuta alipouza nyumba yake na kutokomea yeye na mkewe na kuwaacha watoto wawili wenye umri kati ya miaka 9 na 11 wakikosa mahala pa kuishi.
Akizungumzia sakata hilo kijijini hapo, Mwanaharakati wa haki za Binadamu, Yasin Yuta, alisema majirani waligundua baada ya kusikia kelele za mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Erasto Emmanuel (11) aliyekuwa amefungiwa ndani na kukaa kwa siku tano.
Alisema baada ya kumfungulia mtoto huyo ndipo ilipobainika kuwa nyumba hiyo ilikuwa imeshauzwa huku mtoto akiwa ndani na ndipo mnunuzi alipofunga na kufuli bila kujua kama kuna mtoto ndani huku watoto wengine wakiwa kwa ndugu zao ambao pia hawakuelezwa kama nyumba imeuzwa.
Nyumba hiyo iliuzwa kwa Dati Nsagaje kwa gharama ya shilingi 750,000/= ikiwa ni nyumba mbili pamoja na kiwanja ambapo mnunuzi huyo alilipa kianzio cha shilingi laki nne biashara iliyofanyika tangu April 26 mwaka huu na kiasi kilichobaki wakiwa wameahidiana kulipana Mwezi Mei 15, Mwaka huu.
Wahanga wa tukio hilo ambao ni watoto walisema hawakuwa na taarifa zozote za kuuzwa kwa nyumba wanayokaa ambapo walisikia kuwa baba yao ameenda Sumbawanga kumfuata mke wake ambaye inasemekana aliolewa na mwanaume mwingine.
“Nilikuwa nimelala ndani ambapo nilipoamka asubuhi nilikuta mlango umefungwa kwa nje hata hivyo nilivumilia hadi njaa ilipoanza kuniuma baada ya siku tano nikaanza kupiga kelele ndipomajirani walipokuja kunifungulia na kuniambia nyumba imeuzwa” alisema mtoto Erasto Emmanuel.
Mtoto mwingine aliyetelekezwa ambaye siku ya tukio alikuwa ameenda kulala kwa bibi yake Groli Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Hatwelo alisema siku akiwa anaondoka aliagwa na baba yake ambaye alimwachia shilingi 3000 lakini hakumwambia kama nyumba imeuzwa.
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida na kuonesha kukosa uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kijiji ambao walishiriki moja kwa moja zoezi hilo huku wakiwa wamesaini kama mashahidi na kugonga mhuri wa Serikali ya Kijiji walipoulizwa kuhusiana na sakata hilo hawakuwa na majibu ya kuridhisha.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Hatwelo, Ibrahimu Mponzi, alisema kitendo alichokifanya muuzaji ni cha kawaida kwa sababu ameuza mali yake mwenyewe na kwamba wao kama majirani na serikali ya kijiji hawawezi kuhoji atakako waacha watoto kwa sababu ni mipangilio ya maisha ya kila mtu.
Mbali na mwenyekiti wa Kijiji kuwa shahidi wa upande wa mnunuaji akiwa sambamba na watu wengine wanne akiwepo Mkewe ambaye pia ni Balozi wa nyumba kumi pia waliosaini wengine ni ndugu wa mnunuaji ili hali muuzaji akiwa hana shahidi hata mmoja.
Na Mbeya Yetu
1 comment:
sasa nakulizeni mnanao kipi cha ajabu wakati watu wanakufa na nja huko nyumbani hawana ajira nawana pesa sasa kwa nini asiuze nyumba yake,wakuu wanastarehe utafikiri wafalme halafu cha kushangaza sisi huku ulaya tunalipwa kwa masaa huko kwa mwezi wanalipwa lakini wanatanua utadhani nini je tumejiuliza hili watanzania.
nikweli alichofanya huyu baba si kizuri kabisa kuwaacha watoto ndani ya nyumba na kuiuza nyumba labda kachanganya na kuwauza na wao au labda alikuwa hajui kama wamo humo ndani ya nyumba.
waafrica tulikuwa hatuna tabia hizi za kishenzi na kijinga lakini kwa mazingira ya maisha ndo tunakuwa hivi na halafu kuwaachia wawekezaji waje kwetu na kututafuna na wachache serikalini kufaidika..
nataka kitu kimmoja mjue kwamba SERIKALI YEYOTE ILE HAPA DUNIANI HAIKO KWA AJILI YA WANANCHI TENA WALALA HOI IPO KWA KWA AJILI YAO WENYEWE SERIKALI NA KWA WANANCHI WANAOJIWEZE MATAJIRI.
Kuna siku mtakuja kuyajua haya watanzania wenzangu na kuweza kujisaidia sisi wenyewe sio eeti leo kukaa katika vikao hivi na vile vya vyama na kufunguliwa matawi hapa ulaya ya vyama vyao kwa manufaaa ya nani jeulizeni.
yule yule NY
Post a Comment