ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 1, 2013

BIBI TITI ALIVYOPANGA KUMUUA NYERERE

Bibi Titi na Mwalimu wakihutubia wananchi enzi za TANU.

WIKI iliyopita niliandika juu ya kesi ya uhaini iliyoanza kunguruma Juni 8, 1970 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar.
Niliwataja pia baadhi ya watuhumiwa waliofikishwa mahakamani lakini mtuhumiwa mmoja alishangaza wengi na si mwingine isipokuwa ni Bibi Titi Mohammed (45).
Wengi walishangaa na kujiuliza, mama huyu kweli alitaka kumuua Rais Julius Nyerere? Walijiuliza hivyo kwa sababu enzi hizo mwanamke kujihusisha na kitu kizito kama hicho ilikuwa ni ndoto, lakini yeye alifanya na alimwaga fedha kwa kazi hiyo.
Lakini pia wananchi walishangaa kwa kuwa Bibi Titi aliwahi kuwa waziri na rais wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT). 
Kama ilivyo kwa watuhumiwa wengine ambao walikuwa na majina bandia ya ‘kazi’. Mama huyo naye mahakama iliambiwa alikuwa na majina mengine aliyojiita au kuitwa nayo ambayo ni Mama Mkuu, Mwamba au Anti wakati wa mipango yao ya mauaji na kuipindua serikali ya Nyerere.
Bibi Titi aliyezaliwa mwaka 1926 alikuwa kivutio kila alipokuwa anafikishwa mahakamani kwani wakati wa ujana wake alikuwa mtu wa karibu wa Nyerere.
Alishirikiana wakati wa kudai uhuru na hata baada ya taifa kuwa huru. Ilielezwa kuwa Bibi Titi aliunganishwa kwa Nyerere na dereva mmoja wa teksi ya nyumbani kwao mwaka 1954 na akawa mmoja wa waanzilishi wa chama cha Tanu.
Biti Titi alikamatwa na polisi Oktoba 1969 akiwa na waziri wa zamani wa kazi, Michael Kamaliza pamoja na maofisa wanne wa JWTZ na wote wakafunguliwa mashitaka ya kutaka kumuua na kumpindua Nyerere.
Ushahidi mwingi ulitolewa mahakamani na ilielezwa kuwa alikuwa akimwaga fedha ili kufanikisha mpango huo haramu kutokana na ufadhili wa mtu mmoja ambaye alikuwa nje ya nchi. 
Je, nani alikuwa akimpa fedha? Utapata majibu haya katika toleo lijalo.

GPL

3 comments:

Anonymous said...

History ni part of life,ingekuwa vyema hizi hadithi zitolewe wahusika wakiwa hai ili tujue ina ukweli kiasi gani. Sometime ni kesi za kubambikiwa for political reasons. Anyway,I'm glad baba wa taifa letu alifanya mengi mazuri,na alifariki kwa uwezo wa Mola .Tumesikia mengi lakini mwezeshaji ni Mola,na tunamwombea mapumziko mema. We miss him so dearly! But Mungu kampenda zaidi,alimaliza kazi aliyopewa

Anonymous said...

Nyerere was a dictator, look at Jakaya, he has no one locked up. He will not reach sainthood. Some of his policies were really bad as in very bad.

Anonymous said...

uliyosema ni kweli kabisa mdau number one hapo juu habari hizi ni za uchochezi kabisa yani mtu anakufa ndo zinatolewa hivi sasa kwa nini alivyokuwa yuhai hazijatolewa tena bibi titi alikuwa rafiki mkubwa wa bibi yangu sema tu bibiyangu alikuwa haipendi siasa sana ndo maana hajaijiingiza na bibi titi alikulia pamoja na bibi yangu utafikir ndugu yani acha mtulize tunayoyajua siyo kutuandika ya kubabikiza hivi leo