ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 15, 2013

HATIMAYE BABA ALIYETELEKEZA WATOTO AKAMATWA

.
Watoto Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakifanya usafi katika nyumba wanayoishi 
Hapa ndipo wanapopikia chakula wakati wa usiku kwakweli ni hali ya hatari sana
Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akiwa na watoto hao alipowatembelea nyumbani mara baada ya kuwakosa shuleni mwandishi wetu alipowauliza kwanini hamjaenda shule leo? wakamjibu tulijua leo ni sikukuu ndiyo maana hatujaenda shule,
Hapa wakinawa kutokana na hali ya uchafu waliokuwanayo baada ya kumaliza kufanya usafi nyumba yao
Wakiwa na waalimu wao

8 comments:

Anonymous said...

Mimi kwakweli sielewi mtoto anaishi hivi wakati tunaona kina bakharesa wanatamaba na managari ya mamillioni hata sielewi, yaani hapo ndipo namuelewa kwanini Nyerere alitaka ujamaa, kutoa hii big gap btn rich and poor. Hao wenye magari ya mabillioni hawawezi hatakujitolea kujengea watoto. Je Daimond anaonyesha tu madhahabu. Naamini kuwanjengea hao watoto angalau nyumba yakueleweka aizidi hata millioni 2. Kama inawezakana vijimambo fanaya fanya sie tuchange $10 tuvijumlisha ipatikane heal ya kuwasaidia hao watoto na malazi.

Anonymous said...

Asante mdau pamoja na vijimambo kutupasha. Hawa watoto hawakupenda kuishi hivyo tena nasema wamejitahidi sana chakula wanachokula wanapata wapi? Watanzania wamezisoma hizi habari? Hawa watoto wanatakiwa kwanza kupata elimu na mahali pa kuishi kwa usalama na afya yao. Matajiri wangapi wapo isitoshe wabunge wakiamua kutoa kiwango fulani kwa kipindi cha bungeni lazima watoto hawa wataokolewa, tupunguzeni siasa za ufisadi.

Anonymous said...

Wachangiaji wengine bwana etii Diamond awajengee nyumba! Umesikia wanalala nje? Umesoma au una chuki binafsi. Kaa kule na umaskini wako.. Hawa wanahitaji malezi na mahitaji mengine kama watoto

Anonymous said...

...ndugu yangu hata mimi inaniuma sana sana tu kwa hali hiyo ya hao watoto na kwa kifupi wapo watoto wengi mnoooo ambao ukiangalia kwa makini sana hata hao utaona wana afadhali japo sio vile,Kuchanga sio tatizo kabisa lakini...Je michango itawafikia walengwa au ni kuwavimbisha matumbo watu wengine wanaojiita viongozi huku wakiwa wanajisimamia wao na familia zao tu
Tafakari Chukua Hatua

-Mdau(Paka Jeusi)

Anonymous said...

Hii inasikitisha sana.It is too sad.Hawa watoto wanahitaji msaada.Ni wadogo sana,kupitia hayo waliyopitia.

Anonymous said...

Mimi naona hii taswira inasikitisha ingawa ndiyo maisha ya watoto wengi vijijini,uchafu maeneo wanayoishi,aina ya nyumba na maisha pia,kunawatoto wananwazazi wao na wanishi hivyo kila siku,si jambo zuri hata kidogo lakini ni kweli kabisa nina mifano lakini bila picha wengi hawatoamini nikisema hivyo,kweli wanahitaji msaada lakini siyo tu kutoka kwa bakhresa,au diamond ni kwakila mtu mwenye nia na mapenzi mema.siyo pesa tu hata mtu akichukua muda kuwaosha na kuwapaka mafuta na kuwapa furaha watoto hao ni msaada pia,jirani akijitolea kuwapikia chakula,au kushiriki nao chakula cha mchana na jioni ili pia wapate muda wa kupumzika nakusoma pia ni msaada pia siyo fedha kwa kila kitu.mi nadhani tunao masikini wengi nchini hasa maeneo ya vijijini,na mijini pia lakini hasa vijijini nadhani hivyo.Kujitolea kuwanunulia nguo za shule viatu vya shule,pia mtu anaweza kujitolea kuwasafishia sehemu wanyoishi,majirani kuwaandalia watoto hao chakula au kushiriki naoa badala ya kuwaacha wajipikie,majirani wanaweza kuwaangalia usafi wao vitu kama hivyo sidhani kama hivyo vinahitaji pesa mi nadhnai ni muda na moyo safi wa kujitolea.ni mchango wangu kimawazo sipingani na yeyote hapa. asanteni.

Anonymous said...

tokea hii habari imetoka mbunge wao sugu kachukua hatua gani?

Anonymous said...

Naomba contact mamba please tuque jinsi gain ya kuwasaidia hawa malaika