Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akielezea kuhusu hisia za kutengwa kwa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Waziri Membe alikuwa katika mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri Membe akiendelea na mahojiano hayo, wakati Bi. Fauzia Yusuph wa Channel Ten akirekodi tukio hilo.
Jumuiya ya EAC na talaka rejea
Na TAGIE DAISY MWAKAWAGO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) ameelezea hisia za sintofahamu kuhusu kutengwa kwa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na kuhoji kuwa iwaje nchi yetu itengwe na nini maana ya Jumuiya hiyo?
Aliyasema hayo katika mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, yaliyofanyika ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalijikita zaidi katika kujua msimamo wa Tanzania kidiplomasia wakati huu wa sintofahamu ya Jumuiya hiyo inayoendelea, hususan Tanzania ikionekana kutengwa na nchi za Uganda, Rwanda na Kenya.
“Huu ni muungano wa watu wenye woga,” alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa Jumuiya hiyo ilishawahi kuvunjika mnamo mwaka 1977.
“Jumuiya hiyo ilishawahi kuvunjika na kuungwa tena, na Tanzania hatukuathirika. Tuko tayari kupewa au kutoa talaka, na ikiwezekana labda kutakuwa na talaka rejea,” alisema Waziri Membe. Jumuiya hiyo ya EAC inazijumuisha nchi za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Tanzania.
“Sisi ndio ‘center of gravity’ na ndio soko kubwa la bidhaa katika ukanda wa Afrika Mashariki - tuna rasilimali zaidi ya majirani zetu, tuna utajiri wa ardhi na bandari nne ambazo ni ufunguo wa kutumia bahari kubwa na kufikia nchi nyingine duniani,” alifafanua Waziri Membe. Bandari hizo ni za Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na bandari ya Bagamoyo ambayo ipo katika ujenzi wa kuifanya iwe bandari kubwa ya kimataifa barani Afrika.
Waziri Membe alisema cha kushangaza ni kwamba majirani zetu wanatakiwa kutambua kuwa Tanzania ni nchi ambayo ni mfano pekee wa kuigwa kwa uzoefu wa muungano. “Sisi ni taifa na sio muungano wa makabila matatu au manne,” alisema Waziri huyo.
“Hauwezi leo ukaitaifisha ardhi ya nchi nyingine na kuviacha vizazi vijavyo bila mali,” alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa “kwa vyovyote vile, jumuiya hii ya Afrika Mashariki lazima iende kwa taratibu.”
Aidha, Waziri Membe alienda mbali zaidi na kusema kuwa huenda chokochoko ya kutengwa kwetu inatokana na wivu au gere kwa Tanzania kupeleka majeshi yake huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jambo alilosema huenda halijawafurahisha baadhi ya watu katika Jumuiya hiyo.
Vilevile alisema kuwa kitendo cha Tanzania kukataa ardhi kuwa sehemu ya mali ya Afrika Mashariki huenda pia imepelekea mchango mkubwa kwenye choko choko hizo.
Waziri Membe amewaambia Watanzania kuwa “wakae wakijua kwamba akufuzae hakwambii toka, utaona tuu mambo yanabadilika.”
4 comments:
Mkuu Membe tupo pamoja katika hili,We can do better without them.
Hiyo EAC mwisho wake iwe Namanga, Sirari,au Horohoro. Hakuna kulegeza kamba hakuna kujipendekeza kwao.
Namuunga mkono mwenzangu, Tanzania ijitoe katika East Africa, Tanzania ni nchi yenye utajiri wa kutosha. Zaidi hao majirani wanakuja kwetu na kuchukua kazi zetu..
Ndugu waziri sawa kabisa,kwanza sisi wenyewe cha pili wao. Tusijibebeshe mizigo ya bure!!
Tunahitaji kuiendeleza Tanzania kwa Mtanzania, ya kwao si yetu.
katika muungano kama huo, tutabeba mizigo ya kila aina, kiuchumi wapo chini, kisiasa chini,kitaifa chini, kimaendeleo chini,kiulinzi halikadhalika. achaneni nao watatumia tu! were going to gain nothing,tusisahau ile jumuia iliyovunjika tatizo lilikuwa kama hili kukosa uongozi wa busara. this time let us watch them.!!
Asante Watanzania wenzangu. Nami nimekuwa nikikerwa na kutoelewa kwa nini hao washenzi wanatupotezea muda. The so-called "Coalition of The Willing" ni bunch of insecure, corrupt, and undemocratic leaders wasio na shukrani. Tunawalisha na tumewasaidia in so many ways. It is time for our country to exit from this very irrelevant Union. In the long run they will come back to beg for our assistance, believe me! As the matter of fact, both Kagame and Museveni, won't survive politically in the next 2 years and so is Uhuru, (the ICC is calling-and please, Tanzania should stop defending him!). Tanzania tupo imara na Watanzania tutaendendelea kujijenga na kuilinda nchi yetu. Tafadhali, serikali isipoteze muda kujadili na kulalamika, wacha tujitoe na EAC kabla ya 2014. MUNGU IBARIKI TANZANIA, NA UWABARIKI WATU WAKE NA VIONGOZI WETU.
MSOMI, MAREKANI.
Post a Comment