ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 10, 2013

KINYAIYA AFANYIWA KWELI NA VIBAKA

Stori:Imelda mtema
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Mama Land, kinachorushwa na Runinga ya Clouds ya jijini Dar, Benny Kinyaiya hivi karibuni alikombwa vitu kadhaa kwenye gari lake na vibaka mara baada ya kupaki gari nje ya nyumba yake. na mwandishi wa habari hizi, Kinyaiya alisema kuwa siku ya tukio saa nne usiku aliporejea nyumbani kwake maeneo ya Kinondoni Dar, aliegesha gari nje ya geti na kuingia ndani kuchukua kitu kisha aendelee na mishemishe zake.
Habari zinapasha kwamba, baada ya kuingia wezi hao walitumia fursa hiyo kuvunja vioo na kuiba redio na vitu vingine.
“Inauma sana kwani kilikuwa ni kitendo kama cha dakika chache tu, yaani kuingia ndani na kutoka tu tayari nimeshaibiwa, natamani hata nimkamate mmoja ili nimuoneshe mfano,” alisema Kinyaiya.

1 comment:

Anonymous said...

Jamani sifikirii kama camera(cctv) big deal, ficheni camera hata ndani ya gari kama kwenye nyumba itakuwa haizekani.