ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 16, 2013

KWA WALE WANAOTOKEA PANDE HII YA VIJIBWENI HII INABAMBA NA KAMA UJUI VIJIBWENI NI WAPI NIULIZE

Kutokana na pantoni kuwa mbali basi kwa muda mrefu wananchi wa Vijibweni jijini Dar es salaam wamekuwa wakitumia usafiri huu kuvuka maji ya bahari na kwenda ng’ambo ya pili ambapo mmoja wa wahusika wa boti ameongea na kusema Sumatra huwa wanakwenda kukagua vyombo vyao.

Boti hizi ambazo zimetengenezwa na mbao pamoja na gundi hupewa kasi na mashine ambayo hutumika hata kwenye boti za kisasa ambapo boti zikiwa na life jacket lakini upande mwingine kwa jinsi boti hii ilivyotengezwa, sio rahisi kuweza kupima uzito wa mizigo na watu walioingia kwenye hiyo boti kitu kinaongeza hatari kwenye usafiri huu.

Hawa Wafanyabiashara wanasema wanapata changamoto kubwa maji yakijaa pwani kwasababu kuna mtu amesogeza kifusi hadi karibu na beach hivyo maji yakijaa yanafanya kusiwe na njia wala kituo tena cha abiria kwa ajili ya boti zao, boti moja ina uwezo wa kubeba abiria 40 na kila mmoja hulipa sh 400 ambapo mzigo hauna bei maalum inategemea na ukubwa wake.

Hii ndio mashine ya kuendesha boti nzima
Mafuta yanakaa pale chini kwenye kidumu
Muonekano wa nje wa MV Wastara
Sehemu ya ndani, abiria hukaa kwenye hayo mabenchi ya blue
Boti ikirudi kutoka Vijibweni
Life jacket
Ngazi kuelekea kwenye kivuko
Nikiwa kwenye kituo cha boti kwa mbali naona mradi wa daraja la Kigamboni ukiendelea.Mwanahabari ukitaka kuingia humu kuna mchina anayehusika na kuwaruhusu watu wa habari.

No comments: