Picha mbalimbali juu ni baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika banda la Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakifungua akaunti maalumu ya mwanafunzi 'Platinum Account' baada ya kupewa elimu shuleni hapo.
Baadhi ya maofisa wa TPB (kulia) wakitoa maelezo kwa wanafunzi na kuwafungulia akaunti wanafunzi walipowatembelea shuleni hapo kutoa elimu.
Meneja Mkuu Ukuzaji Amana wa Benki ya Posta Tanzania, Paradise Nkini (kushoto) akizungumza na vyombo anuai vya habari.
Pwani na baada ya hapo elimu kama hiyo itaendelea kutolewa mikoa yote. Alisema elimu hiyo ya kujiwekea akiba kwa wanafunzi inayotolewa na benki hiyo inatolewa sambamba na huduma ya 'Platinum Account' ambayo ni akaunti maalumu kwa wanafunzi iliyoandaliwa kumudu mazingira ya mwanafunzi. "Tumekuja pia kutambulisha akaunti yetu maalumu kwa wanafunzi ijulikanayo kama Platinum, hii imeandaliwa kwa ajili ya wanafunzi na imezingatia kipato chao...kwanza inafunguliwa kwa sh. 5,000 tu, haina makato ya kila mwezi na haina gharama za uendeshaji kama ilivyo kwa akaunti nyingine," alisema Nkini. Aidha alisema sambamba na elimu inayotolewa kwa wanafunzi, TPB inatoa zawadi kwa baadhi ya shule zilizofanya vizuri kitaaluma na kuwazawadia wanafunzi baadhi ya vifaa vinavyowasaidia katika masomo yao. "...Tunatoa zawadi kwa baadhi ya shule hasa zilizofanya vizuri na zile shule ambazo zinahali ngumu za vijijini, tunatoa zawadi za madaftari, tunatoa kalamu na kuwashirikisha wananfunzi waweze kuelewa benki yao vizuri," alisema Nkini akizungumza na wanahabari kwenye viwanja vya shule ya Kibasila.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com





No comments:
Post a Comment