ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 17, 2013

MAONI YA BASALAMA: MAENDELEO NI TABIA SEHEMU YA 2

Wanasema wanafalsafa, unapopenda penda kiasi na unapochukia chukia kiasi. Ukipenda sana utajinyima nafasi ya kuona kasoro na hutoweza kukosoa, na pia ukichukia sana, utajinyima nafasi ya kutambua yaliyo mazuri na hutoweza kushukuru. Inaendele,…….  
Katika kudai maendeleo ya Taifa letu, ni lazima tuwe na fikra tafakuri. Wakati mwingine tujiulize kwa nini hili na lile haliwi. Tuupe mtazamu huria nafasi ya kurejea utaratibu tunaoutumia kila siku wa kutafuta hayo maendeleo.
Ukweli ni kwamba hakuna asiyependa maendeleo. Wote waliojuu na chini, waliondani na nje.
Katika falsafa ningine kama ya Kennedy akisime (Tafsiri): Uliza nini utaifanyia nchi yako, sio nchi yako itakufanyia nini… Pia katika falsafa ya Gandhi inasema (Tafsiri): Mabadiliko huanzia kwako.
Sasa kwa kuzingatia miono hii ya watu wanaoaminika katika harakati za maendeleo ya watu, lazima kutakuwa na mantiki ndani yake.
Hebu turudi nyuma kidogo, tuondoe itikadi za kisiasa na tupime, kwa kujiuliza Je? Na sisi Watanzania tunayo nafasi ya namna hii, na kama tunayo tunaiangalia vipi.
Kabla sijakutengulia jinsi ya kuangalia, ningependa tuangalie miongoni mwa matukio ambayo yanawezakutusaidia kuzipa fikra zetu, hamu ya kuangalia upande wa pili wa uwezekano.  
Taifa letu lina watu mil. 40 (makadirio), lakini wanaolipa kodi ni laki 8 tu. Tegemeo kuu la utowaji huduma la taifa ni kodi. Kodi hii inatakiwa itumike kwenye kuendesha Serikali kwa ajili ya shughuli zake za kila siku na kutoa huduma kwa watu milioni 40 na kuwekeza katika idara na maendeleo ya nchi. 
Mfano mwingine; Pato la taifa katika mwaka 2011 limekuwa kwa asilimia 6.4 na mwaka 2012 limekuwa kwa asilimia 6.9 Pato la wastani la kila mtu limeongezeka kwa asilimia 17.9.  Uchumi unaotegemea kilimo umekuwa kwa asilimia 4.3 kwa mwaka 2012, na mwaka 2011 umekuwa kwa asilimia 3.6  Katika mwaka 2011 na 2012 kilimo kimeweza kuchangia pato la taifa kwa silimia 49.3  Shughuli za ujenzi binafsi zimeongezeka kwa asilimia 16.8 kwa mwaka 2011-12.  Mwaka 2012, barabara mpya kilomita 633.51 zilijengwa na kwa kiwango cha lami, na kilomita 186.84 zilikarabatiwa.
Ikiwa hatua hizi haziingizwi kwenye mkusanyiko wa maendeleo ya Taifa, je tuziweke kwenye kundi lipi? Au ni kweli haya sio maendeleo. Au ni kwa sababu tunachukia sana?  Athari ya hulka ya kuchukia chukia; hata ukikosa cha kuchukia, unaweza kuchukizwa hata na mti kwa jinsi unavyotoa majani au ulivyopinda.
Mimi naona kuna haja kubwa ya Wanzania kubadilika.Vigezo vya kufeli vipo na vitaendelea kuwepo, lakini tusipobadilika sisi wenyewe maendeleo hayo tunayoyataka yataendelea kuwa ndoto; Maendeleo sio halua, utakaa kwenye jamvi na upitishiwe uchukue pande lako, hapana. Maendeleo ni kazi, ili uyapate lazima kila mmoja wetu ashiriki kuyapigania.

1 comment:

Anonymous said...

Kuna tatizo kuu ambalo naliona kwa huyu bwana Basalam, nalo ni ugumu wa kuelewa tofauti kati ya DALILI za maendeleo na MAENDELEO. Bwana Basalama mambo uliyoyataja kwa mfano ongezeko la pato la taifa, Ujenzi wa barabara n.k. Kamwe si Vielelezo sahihi vya KUTHIBITISHA kitu unachokiita MAENDELEO. Ningekushauri ukae chini na ujifunze kuwa NI LAZIMA pawe na UTHIBITISHO usio na UTATA kuwa haya mambo uliyoyataja mfano: ongezeko la pato la taifa au ongezeko la barabara yanachangia KUBADILISHA maisha ya MTANZANIA wa kawaida, jambo ambalo naamini wengi wetu pamoja na wewe tunajua sio kweli. Kwa mantiki hiyo ni vyema ukaacha KUHUSANISHA vitu ambavyo havilingani kwa nia ya KUFIKISHA hoja zisizo sahihi. Basalama kama na hapo hujaelewa labda ujiulize hivi ni watanzania wangapi wanafaidika na ongezeko la pato la taifa?

Lakini sio hivyo tu bado umeendelea na nakishi zako za kusema watanzania wanaolipa kodi ni laki nane (8) tu hizi takwimu umetoa wapi? Hivi wewe unajua kodi ya VAT au hujawahi kuingiza motokari? au unajua kuwa hata yale maduka ya mama na baba yanalipa KODI? Basalama, je unapotembelea Tanzania wewe haulipi kodi kwa manunuzi ya vitu mbalimbali? Je umesahau kodi za bia, sigara, mafuta ya petroli n.k. Jamani tuache kupotosha maana halisi kwa minajili ya kupindisha ukweli. Tatizo la Tanzania ni MATUMIZI yasiyo na VIPAUMBELE.