Adhabu aliyopewa winga Mrisho Ngasa ya kuilipa Simba Sh. milioni 45, itamlazimisha nyota huyo kufanya kazi Yanga bure kwa miaka yote miwili ya mkataba wake, imebainika.
Kwa kuwa Ngasa alikubali kutoa kiasi hicho cha fedha katika akaunti yake ili aruhusiwe kuichezea Yanga, atalazimika kucheza soka miezi 22 na nusu ili kuifanya akaunti yake inone tena kama ilivyokuwa siku chache zilizopita kabla hajawasilisha fedha hizo kwenye ofisi za Shirikisho la Soka (TFF).
Winga huyo wa zamani wa Kagera Sugar, Azam na Simba, ambaye analipwa mshahara wa Sh. milioni mbili kwa mwezi, atalazimika kutoka jasho kwa takriban miaka yote miwili Yanga ili kurejea katika uwezo wa kifedha aliokuwa nao kabla ya Ijumaa iliyopita alipopeleka fedha hizo TFF.
Lakini katika kukabiliana na machungu ya kukwangua akaunti yake, Ngasa ameamua kuweka hadharani namba ya akaunti yake ili mashabiki wampunguzie maumivu na aweze kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani kwa juhudi zaidi.
Ngasa alisema jana kuwa mashabiki na wadau wa klabu hiyo wanaweza kumchangia kwa kutumia akaunti namba 01J2095037800 ya CRDB yenye jina la Mrisho Halfan Ngasa.
“Naomba wanachama na wapenzi wa Yanga walioguswa kunichangia fedha katika akaunti hiyo ili tuwe tumesaidiana kulipa deni hilo,” alisema Ngasa.
Ngasa alifungiwa mechi sita za mashindano na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF baada ya kubainika alisaini mikataba na timu mbili, Simba na Yanga. Pamoja na hayo, mzaliwa huyo wa jiji la Mwanza alitakiwa kurejesha fedha alizodaiwa kuchukua kusaini mkataba wa Simba, Sh. milioni 30 na fidia ya asilimia 50 (Sh. milioni 15), ambazo alilipa Ijumaa jumla ya Sh. milioni 45.
Kufuatia tukio hilo, Ngasa alishauri wachezaji wenzake wawe makini wanapotaka kuingia mikataba na klabu ili yasije yakawakuta kama yaliyomkuta yeye.
“Nawashauri wachezaji wenzangu kwamba, wanapoingia mikataba na klabu, wahakikishe wanakuwa na mawakili, ili wawasaidie kujua kilichomo ndani yake na wasaini mikataba ambayo wanaielewa,” alisema Ngasa, ambaye anaona kwamba alilaghaiwa kusaini mkataba na Simba.
Hata hivyo, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe, alisema katika mahojiano maalum na NIPASHE jana kuwa klabu yao italiwasilisha suala hilo katika vyombo vya sheria endapo Ngasa ataendelea kuwatuhumu kumlaghai.
Sakata la Ngasa linaanzia Agosti mwaka jana alipoukera uongozi wa iliyokuwa klabu yake, Azam FC kwa kwenda kubusu jezi ya Yanga baada ya kufunga bao la ushindi katika nusu fainali ya Kombe la Kagame ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya AS Vita ya DRC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment