
ASALAM alaykum, Bwana Yesu asifiwe. Wapenzi wasomaji wa safu hii ya Kicheni Pati, leo nimekuja na fumbo kubwa bila shaka wakubwa mtanielewa kwani ukiweza kulifumbua utafanikiwa katika ndoa yako miaka yote ya maisha yako.
Mmetoka nyumbani kwa kicheko, kwa shangwe mnasafiri leo hii unatangulia wewe mwanaume kufika kabla ya mkeo, unamuacha nyuma je akiliwa na simba au akivamiwa na majambazi utalia na nani wakati huo uko na mkeo?
Raha ya safari mtoke wote na mfike pamoja, ndoa nyingi zimeshavunjika na wanawake wengi wameshatoka nje ya ndoa zao, hata kama yupo uelewe atakuwa mwizi na uelewe safari anaenda na mtu mwingine.
Nimeshapata mashtaka kutoka kwa wanawake wengi kwamba hawafiki pamoja kwenye safari na waume zao pamoja na raha na starehe ya kubembelezana lakini safari huishia katikati baada ya mwanaume kufika na kuchoka.
Ikiwa una tabia ya kufika haraka ile safari kuna mawili, pengine una tatizo muone daktari haraka lakini pengine ni tabia yako au maumbile yako yanaruhusu hivyo, sasa basi kama unaweza kutembea mwendo mdogomdogo epuka kufika haraka hebu jiulize je, ndoa itakuwa tamu kama utamuacha mwenzako kila siku?
Kila siku utamuona mwenzako anasononeka kwa sababu hafurahii ndoa yake, je, mtakuwa na amani kweli ndani ya nyumba? Ndiyo wivu utaanza kwa kasi kwani mke atakuhisi humpendi na una mwanamke mwingine.
Mke naye ataanza kukudharau na kupata mwanaume mwingine wa kusafiri naye, amani kwa hakika itatoweka, na je waliowasimamia ndoa aibu mtaiweka wapi au watoto wenu mtawapa picha gani? Mambo huanzia faragha lakini baadaye madhara huwa makubwa mpaka kwa watu wanaowazunguka watajua kuwa wanandoa hawa wana jambo.
Ushauri ni kuwa ikiwa baba anafika safari mapema kutokana na maumbile basi ajitahidi kufanya kila njia na ahakikishe mwenzake naye anafika safari kwa vitendo, mikono, macho na kadhalika kwa pamoja.
Viwiliwili vya mwili wako vina uwezo wa kuhakikisha unafika na mwenzako na anaridhika, epuka kuwa mvivu. Mwanaume ukishafika safari yako unasema umechoka unamuacha nyuma mwenzako, wanawake wengi wanalia jamani!
Kama hujamjulia mwenzako ni sehemu gani zinamfanya naye atembee mwendo sambamba na wewe ongea naye kimahaba, mbembeleze, muombe kwa upole akueleze ni wapi anapohitaji umsaidie kufika naye safari kwa pamoja, hii itawasaidia wote kufurahi.
Kuna wataalam wanajua jinsi ya kukufundisha ukafika na mwenzako pamoja, waone ili wakupe mbinu kwani ni nyingi sana.
Mbinu za kuhakikisha unamridhisha mwandani wako, hata mimi ukiniona ‘laivu’ naweza kukufundisha kwani nyingine hazipendezi kuweka hadharani, si unajua haya magazeti pendwa yanawafikia hadi wanafunzi!
Shahada nyingine si za kusoma ni utundu tu na ubunifu wa mwanaume, acha kurukaruka kwani utamaliza mabucha nyama ni ile ile ingawa mapishi yapo ya aina mbalimbali.
Kumbuka kuwa nyama ukishaiweka mdomoni hata iwe imepikwa vipi ladha yake huwa ileile.
Niwaambie ukweli wanaume kuwa mara nyingi ndoa mnazivunja wenyewe halafu mnasingizia wanawake kwamba siku hizi wengi hawajatulia. Je, umemtimizia haki yake ya ndoa? Je, umemfikisha safari yake au wewe unawahi kila siku na kumuacha mwenzako?
Bila shaka fumbo umelifumbua, amka mwanaume leo nimeamua kuwapa ‘laivu’.
Tukutane wiki ijayo.
GPL
No comments:
Post a Comment