ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 15, 2013

Rais Kikwete ataka wananchi wasikilize hotuba zake

Rais Jakaya Kikwete akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 Bw.Juma Ali Simai leo katika uwanja wa CCM Samora mjini Iringa.Vijana wa Halaiki wakitoa burudani kwa kuimba nyimbo mbalimbali zinazohamasisha umoja wa taifa leo wakati wa kilele cha mbio za mwenge wa uhuru katika viwanja vya Samora mjini Iringa.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.Wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2013 wakiingia katika viwanja vya CCM Samora mkoani Iringa leo.
Kiongozi wa mbi za Mwenge wa Uhuru 2013 Bw. Juma Ali Simai akisoma risala ya ujumbe wa wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete leo mjini Iringa.Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakimbiza mwenge wa Uhuru 2013 leo mjini Iringa.

Rais Jakaya Kikwete na mama Salma Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Fenella Mukangara (wa nne kutoka kushoto)

Wananchi wa mkoa wa Iringa na vijana wa halaiki wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Kilele cha mbio za Mwenge leo mkoani Iringa.

Rais Jakaya Kikwete (katikati) akifurahia jambo na wabunge wa Chama Demokrasia na Maendeleo wa Iringa (CHADEMA) akiwemo Mch. Peter Msigwa (wa pili kutoka kushoto) leo wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Iringa.
kwa picha zaidi na maelezo bofya soma zaidi
Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda akiangalia picha za kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere leo mjini Iringa wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2013.Rais Jakaya Kikwete akiangalia picha za kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere leo mjini Iringa wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2013.

Rais Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo kuhusu mfumo wa utajirishaji kutoka kwa Mkururugenzi wa Kampuni ya GODTEC alipotembelea banda lao wakati wa kilele cha mbio za Mwenge mkoani Iringa.

Rais Jakaya Kikwete amewataka wananchi kusikiliza na kuzifuatilia kwa makini hotuba za Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Juius Nyerere, kwa kuwa zina mafunzo yanaweza kusaidia kupata Katiba mpya itakayojibu kiu ya Watanzania wote.

Kadhalika alisema mabadiliko ya katiba ni muhimu na yenye tija kwa jamii na kwa taifa kwa ujumla.

Rais Kikwete alitoa rai hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka 14 tangu kifo cha Mwalimu Nyerere, kilele cha mbio za Mwenge pamoja na wiki ya vijana yaliyofanyika jana Mkoani Iringa.

“Watanzania wenzangu mabadiliko ya Katiba ni muhimu yawe na tija…tusikilize sana hotuba za Mwalimu Nyerere zina mafunzo na zitatii kiu yetu ya kupata Katiba mpya” alisema Rais Kikwete.

Alisema ingependeza mwaka ujao siku ya kuzaliwa mwalimu Aprili 13, mwaka 1922, iwe inaadhimishwa kama siku ya mwalimu badala ya siku ya kifo chake kama inavyofanyika sasa.

Akizungumzia janga la dawa za kulevya, Rais alisema wafanyabiashara wanabadilisha mbinu ya kusafirisha, kuuza na kusambaza kila kukicha lakini serikali pia haijalala.

“Serikali nayo iko makini katika kubadilisha mbinu za kupambana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kwa sababu kila kukicha wanabadilisha mbinu mpya na sisi tunabadilisha mbinu za uchunguzi wa kuwadhibiti,” alisema.

Alisisitiza kuwa ni azma ya serikali yake ya kuanzisha chombo cha kupambana na dawa za kulevya na kwamba hadi mwakani chombo hicho kipya kitakuwa tayari kimeanza kufanya kazi na nguvu kubwa kuliko tume ya kuthibiti dawa za kulevya.

Aliwataka Watanzania kushirikiana na vyombo vya dola kuwataja wanaohusika na biashara hiyo haramu kwa sababu baadhi yao wanawajua na wanaishi nao majumbani.

Kwa upande wa vijana, rais alisema serikali inathamini mchango wao kwa kushiriki katika ujenzi wa taifa na kwamba imeongeza bajeti ya vijana kwa mwaka wa fedha 2013/14.

Alisema serikali inafikiria kuwapa vijana mikopo na kwamba waitumie vizuri katika kujenga uchumi na siyo kwenda kuongeza ndoa zaidi ya moja.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments: