Baada ya wabunge wa Baraza la Wawakilishi kushindwa kukubaliana ilipofika usiku wa manane Jumatau, juu ya bajeti ya matumizi, serikali kuu ililazimika kutangaza kwamba sehemu za idara kadha zitabidi kufungwa.
Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiendelea bungeni kuhusiana na sheria ya kihistoria ya Rais Obama, ya kutowa huduma nafu za afya ambayo imekuwa mashuhuri kwa jina la "Obamacare".
Baraza la wawakilishi linaoongozwa na Warepublican liliidhinisha mswada wa matumizi ya serikali lakini kwa kuambatanisha kufutwa kwa sheria ya Obamacare. Na mara tatu Baraza la Senet linalodhibitiwa na wademokrat limepinga mswada huo.
Kutokanana Bunge kutokubaliana juu ya kupitisha mswada wa kuongeza muda wa matumizi ya serikali kuu sheria ya Marekani inahitaji idara zote ambazo hazina shughuli muhimu kusita kufanya kazi kuanzia Oktoba mosi, yani siku ya Jumanne.
VOA-Swahili
No comments:
Post a Comment