Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Elliasson ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Mwalimu Nyerere Day pembeni yake ni Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi
Balozi Tuvako Manongi akiashiria uzinduzi wa kitabu kuhusu Mwalimu Nyerere
Professa Ali Mazrui akionyesha kitabu kuhusu Mwalimu Nyerere ambacho yeye na Profesa Lindah Mhando wamekiandika
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York Bw. Hajji Khamisi alitumbuiza kwa shairi nzuri la kumuenzi Baba wa Taifa
Wageni waalikwa wakiwa wamemzunguka Professa Mazrui kumsalimia na kununua kitabu
Professa Mazrui na Professa Lindah wakisaini vitabu vya wateja
Mwanamke kanga na haswa ukijua kuifunga. Mgeni wetu Janice Lathen alikuja kutupa tafu anasema anamapenzi makubwa na Tanzania
Balozi wa Cameroon Michel Tommo Monthe
kundi jingine la wageni waalikwa
Balozi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tete Antonio naye akisema machache kuhusu Mwalimu Nyerere
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Balozi wa Nigeria akifuatilia kwa makini tukio hilo
Balozi wa Liberi Marjon Kamara akisoma ratiba ya tukio
Wageni wengine waliokuwapo kwenye tukio hilo
Sehemu ya wageni waalikiwa wakifuatilia tukio hilo
Balozi wa China Liu Jieng katika mazungumzo yake alimuelezea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kama kiongozi aliyekuwa kiungo muhimu cha ushirikiano na urafiki kati ya Tanzania na China na watu wake. Urafiki ambao bado unaendelea hadi leo akaelezea pia ujenzi wa Reli kati ya Tanzania na Zambia iliyojengwa na serikali ya China kuwa ni moja ya kielelezo muhimu cha ushirikiano huo
Balozi wa Afrika ya Kusini naye akielezea pamoja na mambo mengine namna ambavyo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alivyojitolea yeye binafsi na watanzania katika vita vya kuwaondoa makaburu
Balozi wa India Asoke Kumar Mukerji akielezea machache kuhusu uhusiano wa Mwalimu Nyerere na viongozi wa India na namna alivyokuwa muhimili katika kukuza ushirikiano wa Tanzania na India
Balozi wa Jamaica Courtenay Rattary naye hakuwa nyuma kuelezea namna alivyojifunza mengi kwa kupitia maandiko ya Baba wa Taifa na falsafa zake
Mwakilishi wa Kundi la nchi 77 na China ( G77& China) Naibu Balozi Luke Daunivalu akitoa salamu za kundi hilo
Balozi wa Kenya, Macharia Kamau akizungumzwa kwa kiswahili yeye alieleza kwamba kama vitabu vinavyomuhusu Baba wa Taifa vingeandikwa kwa wingi na Waafrika wenyewe, hapa shaka Baba wa Taifa angekuwa na utajiri wa majumba mengi nchini Marekani
No comments:
Post a Comment