CUF yamgomea
Chadema, NCCR vyamvutia pumzi
Chadema, NCCR vyamvutia pumzi
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara,Julius Mtatiro
Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kinatafakari hatua za kuchukua dhidi ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kwa madai ya kutoa taarifa za uongo na kukihukumu kuwamo miongoni mwa vyama vya siasa ambavyo havijawasilisha hesabu kwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa miaka minne, tangu 2009.
Chama hicho kimesema mojawapo ya hatua hizo, ni kumwandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda kumtaka azifundishe kamati za Bunge namna bora ya kufanya kazi zake kama kamati za umma.
Aidha, chama hicho kimesema hakitaitikia wito wa kuhudhuria kikao kilichoitishwa na PAC Oktoba 25, mwaka huu kuzungumzia suala la ruzuku. Kamati hiyo ya Bunge inaongozwa na Mwenyekiti wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano na waandishi wa habari, aliouitisha kwa lengo la kukanusha chama chake kuwamo katika orodha ya vyama vya siasa ambavyo havijawasilisha hesabu zake kwa CAG katika kipindi hicho.
Alisema CUF imetekeleza sheria mbalimbali, ambazo zinataka vyama vya siasa vipeleke hesabu zake ili zikaguliwe na vyombo maalumu vya serikali.
Kwa mujibu wa Mtatiro, hesabu za mwisho ambazo CUF imeziwasilisha kwa CAG ni zinazoishia Desemba 31, mwaka juzi, ambazo ziliwasilishwa Septemba 11, mwaka huu.
Alisema hesabu hizo ziliwasilishwa kwa CAG kupitia barua yenye Kumbukumbu namba CUF/AK/DSM/KM/003/1A/2012/39 iliyokuwa na kichwa cha habari “Kuwasilisha hesabu zisizokaguliwa kwako kwa ajili ya ukaguzi hesabu zinazoishia 31/12/2011.”
Mtatiro alisema hatua hiyo ya CUF ilitokana na maelekezo ya barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyokuwa na Kumbukumbu namba CD.112/123/01A/37, ambayo ilimtaka Katibu Mkuu wa CUF awasilishe hesabu husika zisizokaguliwa kwa CAG.
Hivyo, alisema wamesikitishwa na taarifa za PAC zilizotolewa kupitia Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe, dhidi ya chama chao, ambazo alieleza wamezisikia kupitia vyombo vya habari na kuwataka Watanzania wazipuuze kwa kuwa hazina ukweli wowote.
Katika taarifa yake, Zitto alikaririwa akisema katika kipindi cha miaka minne, serikali ilitoa Sh. bilioni 167 kwa ajili ya ruzuku ya vyama hivyo lakini havijapeleka mahesabu yake kwa CAG.
Mtatiro alisema hesabu za CUF, ambazo hazijawasilishwa kwa CAG ni zile zinazoishia Desemba 31, mwaka jana, ambazo wakaguzi wa ndani na wa nje wamemaliza kuzikagua Julai, mwaka huu.
Alisema hesabu hizo zinasubiri kuthibitishwa na kikao cha Kamati Kuu ya Utendaji ya Taifa cha Oktoba na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF litakalokaa Novemba kabla ya kuziwasilisha kwa CAG Desemba, mwaka huu.
“Hii ina maana kuwa hesabu, ambazo hazijamfikia Msajili ni za mwaka mmoja uliopita na siyo miaka minne kama, ambavyo kamati ya PAC imetangaza,” alisema Mtatiro.
Alisema CUF imesikitishwa na kufadhaishwa na hatua ya PAC kuvihukumu vyama vyote vya siasa wakati jambo hilo ni la chama kimoja kimoja.
Mtatiro alisema mbaya zaidi ni pale Zitto amekuwa akishinda kwenye mitandao ya kijamii akishupalia kuvichukulia hatua vyama, ikiwamo CUF, huku hana taarifa za kina za namna ilivyotekeleza wajibu wake.
Alisema kamati ya Bunge kushinda kwenye mitandao ya kijamii ikihukumu na kutoa taarifa za uongo kwa umma bila hata kuwasiliana na vyama vya siasa ni jambo la kufedhehesha mno.
Mtatiro alisema kamati makini ya Bunge ni ile ambayo inapokea taarifa kutoka pande zote muhimu, inakutana na wadau wote na kisha inajua tatizo liko wapi na kuujulisha umma nani amesababisha uzembe.
“Kwa sababu kamati hii imeligeuza jambo hili kuwa mtaji wa kisiasa na kukitangaza chama chetu kuwa hakikutambua wajibu wake jambo ambalo siyo sahihi, chama chetu kinatafakari hatua za kuchukua ikiwamo kumuandikia Spika ili azifundishe kamati zake namna bora ya kufanya kazi zake kama kamati za umma,” alisema Mtatiro na kuongeza:
“Chama chetu pia hadi leo (jana) hakijapokea barua yoyote ya kuitwa na kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali siku ya tarehe 25 Oktoba kwa hiyo CUF haitahudhuria katika kikao hicho kwa habari za kuitwa kupitia kwenye mitandao ya kijamii.”
Alisema CUF pekee ndiyo ambayo imekuwa ikipata hati safi za ukaguzi wa fedha kila mara tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi na kwamba, haikuwahi kupata doa wala kashfa katika masuala ya fedha.
CHADEMA, NCCR-MAGEUZI HATUJAPOKEA BARUA
Wakati CUF kikiwa na msimamo huo, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alipoulizwa na NIPASHE jana kama chama chake kimeshapata barua ya kuitwa na PAC, alimtaka mwandishi kupata majibu ya swali hilo kwa Afisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.
Makene alipoulizwa na NIPASHE, alisema hadi kufikia jana walikuwa hawajapokea barua yoyote ya kuitwa kwenye kikao cha PAC, badala yake alisema suala hilo wamekuwa wakiishia kulisikia kwenye vyombo vya habari.
Hata hivyo, alisema Chadema wanajiamini, hivyo hawaogopi kwa kuwa wanavyo vielelezo kuthibitisha kuwa hesabu zao zimekaguliwa kwa mujibu wa taarifa ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema nao pia hawajapokea barua ya kuitwa na PAC, lakini akasema kamati hiyo ya Bunge ina mamlaka ya kuwaita kwa mujibu wa sheria.
Hivyo, akasema iwapo wataitwa wataitikia wito huo na kwenda kusikiliza walichoitiwa.
Kauli ya CUF imetolewa siku sita baada ya PAC kumtaka Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kusitisha malipo ya ruzuku kwa vyama vya siasa hadi uthibitisho wa namna hesabu za vyama hivyo zilivyokaguliwa kwa kipindi cha miaka minne, utakapopatikana.
Vyama vinavyopewa ruzuku ya serikali kwa mujibu wa vigezo vya idadi ya wabunge na kura za urais, ni CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP, UDP, DP, APPT-Maendeleo na Chausta.
Jaji Mutungi alikiri mbele ya PAC wiki iliyopita kuwa hajakabidhiwa ripoti yoyote ya ukaguzi wa vyama na kwamba kazi ya ukaguzi ni ya CAG na si ofisi yake.
Kwa upande wake, Msaidizi wa CAG, Benja Majura, alikiri kuwa jukumu la kukagua hesabu za vyama vya siasa liko chini ya ofisi ya CAG, lakini kutokana na ufinyu wa fedha unaoikabili ofisi hiyo, vyama hivyo viliandikiwa barua na kutakiwa kujifanyia ukaguzi vyenyewe na kuwasilisha ripoti kwa CAG.
Wakati CUF ikisema hayo, wiki iliyopita Katibu wa Baraza la Wadhamini wa Chadema, Anthony Komu, Chadema iliwasilisha taarifa zake za fedha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12.
Komu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, alisema hilo linathibitishwa na barua ya Msajili wa Vyama yenye kumb. Na CDA.112/123/01a/37 ya Septemba 4, mwaka jana, iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya siasa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment