Mshindi wa tuzo ya Daudi Mwangosi Absalom Kibanda ambae ni mwenyekiti wa jukwaa la wahariri akibembelezwa na mkewe baada ya kuangua kilio ukumbini mara baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo leo jijini Mwanza.
Na Abdulaziz video,Mwanza
Mhariri mtendaji wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda leo amekabidhiwa tuzo ya Uandishi wa kishujaa na Utumishi uliotukuka ya Marehemu Daud Mwangosi baada ya Mhariri huyo kukumbwa na tukio la uvamizi na kisha kutobolewa jicho na watu wasiofahamika Machi 6 mwaka huu. Kabla ya makabidhiano ya tuzo hiyo wadau wote wa habari wakasimama na kisha kuimba wimbo maalumu wa kumuenzi Marehemu Daud Mwangosi.

Akizungumza na wadau wa habari Jijini Mwanza. Baada ya makabidhiano hayo mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Tido Mhando amewahimiza waandishi wa habari kuendelea kupambana katika jitihada za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa. Kutokana na umuhimu wa tuzo hii ya Marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la machozi lililolipuliwa visivyo September 2 mwaka jana kijijini nyololo mkoani Iringa Mhando akatumia fursa hii kulaani vikali vitendo vya kuminya uhuru wa habari vinavyofanywa na baadhi ya viongozi nchini.
Baada ya kibanda kukabidhiwa tuzo hiyo pamoja na hundi ya shilingi
millioni kumi akawapa moyo wa ujasiri waandishi wa habari kote nchi wa
kutonyamazishwa wakati wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao licha ya kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo zikiwemo za
vitisho.
Kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya habari nchini wadau wa habari wakiwemo wakongwe katika fani hii hawakubaki nyuma kuelezea mitazamo yao kuhusu uelekeo wa sekta hii. Tuzo za uandishi wa kishujaa na utumishi uliotukuka ya Marehemu Daud Mwangosi itakuwa ikitolewa kila mwaka ili kutambua michango mbalimbali inayotolewa na waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kukabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi Bw Tido Mhando wa tatu kulia akimkabidhi mshindi mfano wa hundi ya Tsh milioni 10 Absalom Kibanda tuzo yenye thamani ya Tsh milioni 10,0000 katikati ni mjane wa Mwangosi Itika Mwangosi wa kwanza kushoto ni makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanji na rais wake Keneth Simbaya.
No comments:
Post a Comment