Mhe. Liberata Mulamula akiwasili kwenye Ibada ya Mavuno Usharika wa Kikristu wa Kiswahili Minneapolis, Minnesota na kupokelewana Mchungaji wa Usharika huo Andrea Mwalilino. Katikati ni mshereheshaji wa shughuli ya Mavuno Bw. Gracious Msuya. Ibada hiyo ilifanyika Jumapili tarehe 3 Novemba 2013.
Mhe. Liberata Mulamula akizungumza na waumini wa usharika huo ambao wengi wao ni Watanzania waliofurika kwa wingi wakati wa sherehe hizo za mavuno tarehe 3 Novemba 2013.
Mchungaji Mwalilino na sehemu ya waumini akiongoza wimbo wakati wa Ibada ya Mavuno ya usharika huo.
Blanketi likiuzwa kwenye mnada wakati wa sherehe za mavuno usharikani hapo ambapo ahadi na makusanyo ya mavuno yaliyopatikana ilikua jumla ya dola za kimarekani 2,500.
Muendeshaji wa mnada huo Smart Baitani akipita kusalimia meza kuu baada ya kufunga mnada rasmi.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Mhe. Kjell Berg, Balozi wa Heshima wa Tanzania Jimboni Minnesota akiwasalimia Watanzania wakati wa sherehe za mavuno kwenye kanisa la Usharika wa Kikristu wa Kiswahili, Minneapolis Minnesota.
Balozi Mulamula aliyeambatana na mumewe Bw. George Mulamula wakiagana na Mhe. Kjell Berg baada ya sherehe hizo za mavuno kukamilika.
Watanzania na Marafiki wa Tanzania waliokusayika kwenye hafla ya chakula cha usiku nyumbani kwa Bw. Meshak Balira New Hope, MN kwenye picha ya pamoja na Mhe. Balozi Liberata na Bw. George Mulamula baada ya chakula na maongezi.
osiah Kibira mtayarishaji wa Filamu za Kiswahili za BongoLand I,II, III na IV akimzawadia Balozi Mulamula filamu hizo ambazo alisema zimesambazwa Vyuo Vikuu vinavyofundisha Kiswahili nchini Marekani na nje ya Marekani.
3 comments:
thanks giving day ndo sikuku ya mafuno siyo jamani kweli mnajisahaulia sikuu kuu zenu mnajishoboa na za wenzenu ndo na wafurahi mnavyokuwa assimilated.mbona huko nyumbani hamji mkasherehekea siku zenu kwani hakuna wakulima na mbona hamuwaoni red indian kusherehekea hizi sikukuu mbapo nchi hii ilikuwa ndo yao wakanyanganywa. kuelimu jamani si mchezo
Huyu anoni hapo juu anaonekana sio mkristu, ungekuwa mkristu wa dhehebu lolote, kama katoliki, lutheran etc Tanzania ungeelewa maana ya Jumapili ya Mavuno, inasheherekewa na makanisa mengi Tanzania. yes tuko ugenini lakini sherehe zetu bado tunashehereakea ugenini, please reserch before you comment in public
Bila shaka huyo mtoa maoni wa kwanza bado yuko gizani na hajui lolote juu ya sikukuu ya mavuno katika matoleo ya kanisa.Tumemsamehe bure maana hajui alisemalo.
Nasahihisha kidogo kwenye maelezo ya makusanyo ya sikukuu hiyo. $2500 ni makusanyo kwa ajili ya mnada wa vitu vilivyotolewa, na $ 4235 zilikusanywa kwa waliotoa pesa taslimu.Hivyo kulikuwa na jumla ya makusanyo ya $6735.hayo ndio matoleo yote.Mungu awabariki wote waliomtolea Mungu kwa upendo.
Post a Comment